Iwapo Sessions atathibitishwa na kamati hiyo shauri lake litapelekwa kwenye baraza lote la Seneti.
Wakati wa mahojiano, wademokrat walioko katika kamati hiyo wana uwezekano mkubwa wa kuelezea kupinga kwao amri za kiutendaji za uhamiaji zilizotolewa na Trump. Sessions ana sifa ya kuchukua misimamo mikali katika masuala ya uhamiaji, kitu ambacho amekuwa akimshauri rais.
Kaimu mwanasheria mkuu afukuzwa
Siku ya Jumatatu, Rais Trump amemfukuza kazi kaimu Mwanasheria Mkuu, Sally Yates baada ya kuhoji uhalali wa kikatiba wa amri yake kuwazuia wasafiri kutoka nchi saba zenye waislamu wengi na Yates kukataa kuitekeleza.
Kukataa kwa Yates kutekeleza amri hiyo ni ishara haitabadilisha kitu hasa ukizingatia kuwa Sessions ataendeleza sera hiyo atakapoapishwa kama inavyo tarajiwa.
Ikiwa Kamati ya Sheria katika baraza la Seneti itampitisha Jumanne, Sessions anaweza kukubaliwa kushika wadhifa huo na baraza lote la Seneti katika siku chache.