Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 02, 2022 Local time: 19:37

Mgeuzi ya mfumo wa kodi Tanzania yahitajika ili kuleta maendeleo


Bunge la Tanzania

Serikali ya Tanzania imeaswa kuwa kama haitabadilisha njia za kukusanya kodi, uwezekano wa nchi kupiga hatua ni mdogo kwa kuwa hazikusanywi ipasavyo.

Taarifa za Wizara ya Fedha nazo zinaonyesha ‘payee’ imeshuka, VAT kwa bidhaa zinazoagiziwa kutoka nje imeshuka na mapato ya bandari nayo yameshuka kwa asilimia 13.

Mbunge wa Nzega Mjini (CCM) amesema mlipa kodi mkubwa nchini ambaye ni TBL, ameshusha kodi yake kwa Sh bilioni 50 katika mwaka wa fedha 2016/17.

Amesema kuwa tayari mpaka sasa biashara 7,700 zimeshafungwa, ajira nazo zimepotea.

Hussein Bashe amesema bungeni Jumatano kuwa tatizo hapa ni wingi wa kodi ingawa sisi hatuelewi. Serukamba amesema hapa jana, kwamba katika kila biashara binafsi, Serikali ni mbia kwa asilimia 30.

Taarifa za Wizara ya Fedha zinaonyesha biashara laki mbili zimefunguliwa ingawa ‘athari’ ya kufunguliwa kwa biashara hiyo hatuioni kama tunavyoona ‘athari’ kwa biashara kufungwa, amesema mbunge huyo.

"Dk. Mpango sina shaka na taaluma yako, nakuomba muwaite wafanyabiashara wakubwa kama TBL mzungumze nao kwa sababu siku zote kodi haikusanywi kutoka kwa watu masikini, bali inakusanywa kwa wafanyabiashara wakubwa," amesema Bashe.

“Nawaambia kabisa, sitavumilia kulisema hili kwa sababu kulitambua hakuhitaji kuwa na Phd au uprofesa,” Bashe ameongeza.

Kampuni ya Cocacola Kwanza imepunguza wafanyakazi 130 baada ya uzalishaji kushuka na kusema hiyo ni dalili ya hali ngumu inayowakabili wafanyabiashara nchini.

Imeelezwa kuwa baadhi ya wafanyabiashara wanaoagiza bidhaa kutoka nje ya nchi, wameanza kuitumia Bandari ya Mombasa, Kenya kwa kuwa kodi zimekuwa nyingi nchini.

Kwa mujibu wa repoti katika mwaka wa fedha 2014/15, asilimia 1.4 ya bidhaa zilizoingia nchini Kenya kupitia Bandari ya Mombasa, zilitakiwa kuingia Tanzania na mwaka wa fedha 2016/17, asilimia 2.2 ya bidhaa zilizoingia nchini humo zilitakiwa kupitia Tanzania.

Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete (CCM), aliitaka Serikali ibuni mbinu mpya za kukusanya kodi badala ya kuendelea kuwabana wafanyabiashara wadogo ambao wengi wao wameanza kufunga biashara.

Pia alisema Watanzania kwa sasa wana maisha magumu, huku akionekana kutoridhishwa na kauli ya Serikali inayosema uchumi unazidi kukua wakati wananchi wanazidi kuwa na maisha magumu.

Kwa mujibu wa Ridhiwani, uchumi bora lazima uendane na maisha bora waliyonayo wananchi.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG