Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 20:02

Ufaransa yaonya magaidi wanaojaribu kuvuruga uchaguzi wa urais


Risasi imeacha athari katika dirisha la duka ambalo liko katika barabara ya Champs Elysees boulevard huko Paris, April 21, 2017, baada ya shambulizi la kigaidi
Risasi imeacha athari katika dirisha la duka ambalo liko katika barabara ya Champs Elysees boulevard huko Paris, April 21, 2017, baada ya shambulizi la kigaidi

Maafisa wa ngazi ya juu wa Ufaransa wamesema Alhamisi mashambulizi ya risasi jijini Paris na mpango wa mashambulizi uliodhibitiwa na polisi huko Marseilles mapema wiki hii ni sehemu ya jitihada za vikundi vya Kiislamu vyenye siasa kali kuvuruga matokeo ya uchaguzi.

Polisi wanawasiwasi wa kuwepo mipango ya mashambulizi ya kigaidi- ukiwepo uwezekano wa kufanyika mashambulizi siku ya uchaguzi utakaofanyika Jumapili.

“Wanataka kuvuruga maisha ya kisiasa ya Ufaransa kwa kuleta vurugu katika mtiririko au hata mipangilio ya uchaguzi,” Thibault de Montbrial, aliyekuwa mkuu wa taasisi ya wataalamu katika wizara ya mambo ya nje, kituo ambacho kinafanya uchambuzi na kutoa dira ya siasa na uchumi, ameliambia gazeti la Ufaransa la Le Figaro.

Vyombo vya usalama vya Ufaransa vimesema mshambuliaji wa bunduki, aliyetajwa jina lake mara moja na kikundi cha kigaidi cha Islamic State kupitia shirika lake la habari Amaq kama ni Abu Yousif al-Bajiki wa Ubeljiji, alilitupia risasi gari la polisi lililokuwa limepaki katika eneo la Champs Élysées, zilizowapata polisi watatu na mtalii mmoja wakati wa shambulizi hilo nje ya duka la nguo la Marks and Spencer.

Mtu huyo alikuwa anasilaha aina ya Kalashnikov na alipigwa risasi na kufa hapo hapo wakati akijaribu kukimbia. Mmoja ya maaskari hao alikufa palepale penye tukio hilo.

Mwanzoni walioshuhudia tukio hilo wamerepotiwa kusema askari huyo aliyekufa alipigwa risasi wakati akiwa ndani ya gari lake, ambayo lilikuwa limeegeshwa katika eneo la barabara lenye mataa ya kuongoza magari. Mtu huyo mwenye silaha alishuka kwa ghafla kutoka kwenye gari jingine na bila ya kusita akawa anarusha risasi.

Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani ya Ufaransa amesema inawezekana kulikuwa na zaidi ya mshambuliaji mmoja katika shambulizi hilo na kuthibitisha kuwa lengo lilikuwa “kuwashambulia kwa makusudi” polisi. Mshukiwa wa pili alijisalimisha yeye mwenyewe Ijumaa kwa polisi wa Antwerp, Ubeljiji.

Rais wa Ufaransa Francois Hollande amefanya mkutano wa dharura na washauri wake wa ngazi za juu na wakuu wa usalama Ijumaa kuzungumzia jinsi gani wanaweza kuulinda uchaguzi wa Jumapili. “Maombolezi ya kitaifa yatafanyika kumuenzi afisa wa polisi aliyeuawa katika shambulizi lisilo na msingi,” kiongozi huyo wa Ufaransa aliwaambia baadae waandishi.

Shambulizi lilipangwa mapema

Mtaalamu wa kupambana na ugaidi wa Uingereza Olovier Guitta ameiambia VOA uharaka usiokuwa wa kawaida uliofanywa na kikundi hicho cha IS katika kudai wamehusika na shambulizi hilo unaonyesha kuwa mashambulizi haya sio kwamba tu “yalishawishiwa” na kikundi hicho cha kigaidi lakini pia yalikuwa yamepangwa na watu hao.

“Uwezekano wa kuwepo mashambulizi zaidi ya kigaidi katika uchaguzi wa urais Ufaransa ni mkubwa sana,” amesema.

“Watu wenye misimamo mikali ya kidini watajaribu kuingilia kati uchaguzi,” ameongeza kusema Guitta, ambaye anaendesha taasisi ya GlobalStrat, Kampuni ya kushauri masuala ya hatarishi iliokuwa na makao yake London.

Shambulizi la Alhamisi lilitokea wakati wagombea rasmi 11 katika uchaguzi walipokuwa wanafanya majadiliano mubashara katika televisheni ya kitaifa ya Ufaransa. Baadhi ya wachambuzi wa kisiasa walitabiri kuwa shambulizi hilo linaweza kumpandisha chati katika uchaguzi unaokuja, Marine Le Pen, mwanasiasa mwenye umaarufu wa mrengo mkali wa kulia ambaye amekuwa akisema uhamiaji unatishia usalama na utamaduni wa Ufaransa.

Wapinzania wa Le Pen wanasema wenye siasa kali za kidini wanataka ashinde, wakidai kuwa msimamo wake mkali dhidi ya sera za uhamiaji ambazo anataka kuzileta zitazidi kuvisaidia vikundi vya wapiganaji wa Islamic State kupata wafuasi zaidi. Lakini wale wanaomsapoti wanakanusha madai hayo.

Wakati wa majadiliano Le Pen, ambaye alikuwa anapewa kura za maoni kuongoza katika orodha ya wagombea katika raundi ya kwanza ya uchaguzi Jumapili, lakini ambaye katika siku za hivi karibuni amekuwa akipoteza umaarufu, alisisitiza wito wake kuwa Ufaransa lazima iondokane na Schengen inayoruhusu uhuru wa uhamiaji na kuanzisha sheria zenye kudhibiti zaidi watu kuvuka mipaka.

“Uhamiaji unaongezeka mbele ya macho yetu. Dhibitini mipaka yetu, kama sihivyo hatutoweza kukabiliana na wimbi hili la wahamiaji!” amesema.

Wakati habari za shambulio hilo zilipotangazwa, wagombea walijaribu kila mmoja kumshinda mwenzie kwa kuonyesha hatua kali wanazopendekeza katika kuilinda ufaransa kutokana na ugaidi.

“Inatosha kuona tulivyokuwa sio makini na inatosha kuonyesha namna tulivyozembea,” Le Pen aliweka wazi. Mgombea mconservative Francois Fillon alipendekeza kuanza kukamatwa kwa washukiwa walioko katika orodha ya magaidi, mfano wa mshambuliaji huyu wa Alhamisi.

Maafisa wa polisi walifanya upekuzi karibu na nyumba ya mshukiwa huyo ambaye alirusha risasi kwa polisi katika Eneo la Paris la Champs Elysees, huko Chelles Aprili 21, 2017.

Ushindani mkali wa kinyang’anyiro cha urais

Kura za maoni (Pollsters) zimekuwa zikisema kwa wiki nyingi sasa kuwa mbio za urais ni zenye ushindani mkali kati ya wagombea wanne wa juu, Le Pen, Fillon, mwenye siasa za mrengo wa kati na Emmanuel Macron mwenye kutaka kuendelea na uanachama wa Umoja wa Ulaya na mgombea wa mrengo wa kushoto Jean-Luc Melenchon. Wachambuzi wanasema kuwa jambo kubwa litakalo tokea dakika za mwisho karibu na uchaguzi zinaweza kubadilisha matokeo ya uchaguzi.

Macron, ambaye aliwahi kuwa waziri wa uchumi ambaye anauzoefu mdogo sana kwenye masuala ya usalama, alikuwa anachunga kauli yake kuliko Le Pen na Fillon wakati wa majadiliano Alhamisi, akitahadharisha kuwa Ufaransa itabidi iendelee kukabiliana na ugaidi kwa miaka mingi inayokuja. Katika kura za maoni katikati ya wiki Macron alielekea kumpita mpinzani wake Le Pen.

Siku ya Jumanne, polisi wa Marseilles waliwakamata watu wawili wakiwashuku kuwa wanapanga jaribio “lililokuwa liko njiani” nchini Ufaransa. Polisi wamesema kuwa wamegundua mabomu na silaha katika nyumba inayowahusisha washukiwa hao. Wagombea urais walikuwa wametahadharishwa na wakuu wa usalama kuimarisha ulinzi wao binafsi.

Mkuu wa Usalama wa Ufaransa amesema wanawashuku watu hao wawili, wote wakiwa ni wazaliwa wa Ufaransa ambao wana miaka ishirini, walikuwa katika maandalizi ya kufanya mashambulizi wakati wa uchaguzi.

Katikati ya wiki Macron na Le Pen walibishana juu ya suala la hatua za usalama zinazopaswa kuchukuliwa katika mahojiano ya radio kila mmoja peke yake. “Leo Uislamu wa siasa kali umeanzisha vita na hakuna hatua zinazochukuliwa kuzuia hatari hii,” Le Pen amesema kupitia Radio ya Ufaransa RFI.

MMacron akajibu kupitia raid RTL: “Hakuna kitu kama kutokuwepo kwa hatari kabisa… Nasikia Le Pen…mtu yoyote anayesema kuwa anaweza kuondoa hatari kabisa sio makini na ni muongo.”

Miaka miwili iliyopita, Chama cha Le Pen cha National Front kiliongoza katika raundi ya kwanza ya wiki ya chaguzi za mikoa baada ya shambulizi la Paris 2015 ambalo lilisabibisha vifo vya watu 130.

Lakini tukio ambalo inawezekana lilikinyanyua chama cha National Front, hali hiyo haikuendelea katika raundi ya pili na chama hakikushinda udhibiti wa siasa katika mkoa wowote.

XS
SM
MD
LG