Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 09, 2022 Local time: 22:10

Korea Kaskazini yaonyesha utayari wa jaribio la nyuklia


Wananchi wa Korea Kusini wanaangalia televisheni inayoonyesha picha za satellite za kituo cha nyuklia cha Korea Kaskazini

Picha za Satellite za eneo la majaribio ya nyuklia la Korea Kaskazini zinaonyesha harakati zinazoweza kuashiria maandalizi ya majaribio ya silaha za nyuklia, kwa mujibu wa Chuo Kikuu cha John Hopkins cha Marekani – Taasisi ya Korea jijini Washington.

Repoti moja Ijumaa kutoka Progamu ya 38 Kaskazini, mradi wa mtandao wa taasisi hiyo ambao umejikita katika kuchambua maendeleo ya utengenezaji wa nyuklia wa Korea Kaskazini, imesema eneo hilo linaonekana linauwezo wa kufanya jaribio la nyuklia wakati wowote watakapo pokea muongozo kutoka Pyongyang.

38 North (www.38north.org) ni programu ya Taasisi ya Marekani na Korea katika Shule ya John Hopkins ya masomo ya juu ya kimataifa, ambayo inatoa taarifa na uchambuzi wa masuala yanayohusu Korea Kaskazini na Korea Kusini.

Picha ya eneo hilo la majaribio, zimeonyesha harakati mpya karibu na eneo hilo la kuingilia Kaskazini.

Picha hizo zimekadiriwa kuonesha angalau viberenge vitano vya machimboni, trela lenye mashine moja ndogo na eneo lilofunikwa kabisa ambalo linaweza kuwa limeficha mashine ndani yake.

Programu ya 38 Kaskazini imesema ujazaji maji ambao unatumika ilikuweka uwastani wa hali ya hewa kwa ajili ya mali ghafi za nyuklia unaonesha umesitishwa.

Pia picha za eneo kuu la utawala la kituo hicho cha nyuklia cha Korea Kaskazini zimeonyesha lori dogo likiweko katika uwanja wake, pamoja na “vitu vingine kadhaa ambavyo havikuweza kutambuliwa na pia harakati ambazo hazikufahamika zinahusiana na nini.”

Wachambuzi wamesema vitu hivyo vinawezekana vikawa ni mahitaji muhimu au vifaa vilivyofunikwa na maturbali.

Mchambuzi huyo ambaye anahusika na repoti hiyo, Joseph Bermudez na Jack Liu, wamesema haikuweza kufahamika iwapo alama hizo mpya zinaashiria “ni mbinu ya kusitisha” kwa muda kabla ya jaribio hilo la nyuklia kuendelea, au ni hatua pana zaidi na ya muda mrefu ya “Kusitisha” operesheni za kawaida katika kituo hicho.

Korea Kaskazini tayari imeshafanya majaribio ya silaha za nyuklia tano tangu 2006, yakiwemo mawili mwaka jana.

XS
SM
MD
LG