Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Oktoba 04, 2024 Local time: 00:12

Serikali ya Senegal yapiga marufuku matumizi ya mtandao wa Tik Tok


Mtandao wa kijamii wa Tik Tok, November 7, 2019. REUTERS/Dado Ruvic/Illustration
Mtandao wa kijamii wa Tik Tok, November 7, 2019. REUTERS/Dado Ruvic/Illustration

Waziri wa mawasiliano amesema hayo hii leo, siku chache baada ya kuweka vizuizi kwa huduma ya internet, huku maandamano yakiwa yanaendelea nchini humo.

Taarifa ya waziri wa habari inasema kwamba hatua ya kupiga marufuku Tik Tok inatokana na mtandao huo kutumika na watu wenye nia mbaya kusambaza ujumbe wa chuki na wenye lengo la kutatiza usalama wa Senegal na kupelekea nchi hiyo kuyumba.

Huduma ya internet imezuiawa nchini Senegal tangu Jumatatu, na serikali imetumia hoja ya usalama na utulivu wa taifa hilo la Afrika magharibi kutekeleza hatua hiyo.

Serikali imechukua hatua hizo baada ya kiongozi waa upinzani Ousmane Sonko kufunguliwa mashtaka ya kupanga maandamano dhidi ya serikali, kupanga njama za uhalifu, miongoni mwa mengine.

Wafuasi wa kiongozi wa upinzani Ousmane Sonko wakiandamana katika mitaa ya Dakar Jumanne Machi 14, 2023. (AP Photo/Sylvain Cherkaoui)
Wafuasi wa kiongozi wa upinzani Ousmane Sonko wakiandamana katika mitaa ya Dakar Jumanne Machi 14, 2023. (AP Photo/Sylvain Cherkaoui)

Senegal imeshuhudiwa maandamano ya mara kwa mara mwakaa huu, wanasiasa wa upinzani wakimshutumu rais Macky Sall kwa kile kile wametaja kama kumlimbikizia mashtaka ya uongo Sonko, ili kumzuia kugombea urais katika uchaguzi mkuu, Februari mwaka ujao 2024.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters.

Forum

XS
SM
MD
LG