Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 08, 2024 Local time: 14:36

Mwanasiasa wa upinzani nchini Senegal aanza mgomo wa kula


Kiongozi wa upinzani nchini Senegal Ousmane Sonko
Kiongozi wa upinzani nchini Senegal Ousmane Sonko

Mwanasiasa maarufu wa upinzani nchini Senegal Ousmane Sonko Jumapili alisema ameanza mgomo wa kula akiwa chini ya ulinzi wa polisi baada ya kukamatwa wiki iliyopita, huku mawakili wake wakilaani kukamatwa kwake.

Mwendesha mashtaka wa Senegal Jumamosi alitangaza mashtaka mapya saba dhidi ya mwanasiasa huyo, mkosoaji mkubwa wa Rais Macky Sall ambaye amekabiliwa na msururu wa kesi ambazo anadai zinalenga kumuondoa kwenye uwanja wa siasa.

“Huku nikikabiliwa na chuki nyingi, uongo, dhulma, mateso, nimeamua kustahamili”, Sonko aliandika, akiwaomba “wafungwa wote wa kisiasa” kuungana naye katika mgomo huo.

Anatarajiwa kuhojiwa na jaji leo Jumatatu.

Katika mkutano na waandishi wa habari jana Jumapili katika mji mkuu wa Dakar, mawakili wa Sonko walisema mamlaka hajiheshimu haki zake.

Mmoja kati yao, raia wa Ufaransa Juan Branco alifika kwenye mkutano na waandishi wa habari licha ya hati ya kumkamata iliyotolewa na waendesha mashtaka wa Senegal tarehe 14 Julai.

“Tumekuja hapa kuwaambia kwamba hatuogopi,” Branco alisema.

“Ninaapa kumtetea Ousmane Sonko, ambaye anabeba matumaini ya wananchi wote, na kwa hivyo, ya wanadamu wote.

Forum

XS
SM
MD
LG