Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Agosti 15, 2022 Local time: 04:49

Rais Trump anapanga kuipiga marufuku App ya Tik Tok kutoka China ifikapo Agosti 15


App ya Tik Tok kutoka China ambayo Rais Trump ana nia ya kuizuia ifikapo Agosti 15,2020.

Rais Trump alisema Jumatatu hatojali kama kampuni ya Microsoft inajiongeza kuichukua APP ya Tik Tok lakini ununuzi huo utatakiwa kukamilika ifikapo Septemba 15 mwaka huu

Rais wa Marekani Donald Trump alisema Jumatatu kwamba atapiga marufuku APP maarufu ya video iitwayo Tik Tok ya China ifikapo Septemba 15, vinginevyo kampuni ya Microsoft au kampuni nyingine yeyote ile ya Marekani iinununue kama uamuzi wake.

Rais huyo kutoka chama cha Republican alisema wiki iliyopita kwamba atapiga marufuku APP hiyo ambayo inamilikiwa na kampuni ya kichina ya ByteDance kwa sababu ya wasi wasi wa usalama. Rais Trump alisema Jumatatu hatojali kama kampuni ya Microsoft inajiongeza kuichukua APP hii lakini ununuzi huo utatakiwa kukamilika ifikapo Septemba 15.

Katika taarifa Microsoft ilithibitisha kwamba mkurugenzi wake mkuu alikutana na Rais Trump na alikuwa na nia ya dhati kuinunua kampuni ifikapo tarehe ya mwisho iliyotolewa. Trump aidha alisema angependa kuona kiasi fulani cha fedha zitakazolipwa katika makubaliano hayo ya ununuzi kinaenda kwa wizara ya fedha ya Marekani.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG