Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 19, 2024 Local time: 02:01

Serikali ya Kenya yafunga akaunti zinazoshukiwa kuwasaidia Al-shabab


Kundi la wanamgambo wa Al-Shabab la nchini Somalia
Kundi la wanamgambo wa Al-Shabab la nchini Somalia

Serikali ya Kenya imefunga akaunti 86 za watu binafsi na taasisi zinazoshukiwa kuyasaidia msaada wa kifedha makundi ya kigaidi likiwemo la al-Shabab lenye makao makuu yake nchini Somalia.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:31 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Taarifa ya serikali iliyotolewa Jumatano kupitia gazeti rasmi la serikali iliyataja mashirika yaliyoshukiwa kulisaidia kundi la al-Shabab ni pamoja na Hawala ambalo kwa miaka mingi iliyopita lilikuwa likihusika na biashara ya usafirishaji fedha kutoka mataifa ya nje hadi mjini Nairobi, Kenya na hatimaye kufika nchini Somalia.

Mji wa Nairobi ulikuwa ni makao makuu ya mashirika hayo ya usafirishaji fedha. Baadhi ya akaunti nyingine zilizofungwa ni zile zilizopo ndani ya makampuni hayo kama vile Dahab Shir, Juba Express, Amal na Amana. Pia mashirika ya haki za binadamu yaliyofungiwa akaunti zake ni pamoja na Haki Afrika, Muhuri mjini Mombasa pamoja na makampuni kadhaa ya usafirishaji mabasi kama vile G-Couch na E-Couch.

Shambulizi katika chuo kikuu cha Garissa
Shambulizi katika chuo kikuu cha Garissa

Uamuzi uliochukuliwa na serikali ya Kenya kufunga akaunti hizo unafuatia shambulizi la kigaidi lililofanyika April 3, 2015 katika chuo kikuu cha Garisa kilichopo kaskazini-mashariki mwa nchi hiyo. Shambulizi lilisababisha vifo vya wanafunzi 150 na kundi la wanamgambo wa al-Shabab walidai kuhusika kwa shambulizi hilo.

Kundi la wanamgambo wa al-Shabab limekuwa likifanya mashambulizi mara kwa mara nchini Kenya likidai ni kulipiza kisasi kwa nchi hiyo kupeleka wanajeshi wake nchini Somalia ili kuisaidia serikali ya Somalia kulitokomeza kundi la wanamgambo wa kigaidi la al-Shabab.

XS
SM
MD
LG