Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 10, 2022 Local time: 11:26

Sauti ya Amerika, VOA, Yaadhimisha miaka 79


Miaka 79 ya VOA.

Sauti ya Amerika, VOA, leo Februari mosi, imetimia miaka 79 tangu kuanzishwa.

Matangazo yake ya kwanza mwaka 1942 hayakuwa makubwa – dakika 15 za matangazo ya masafa mafupi kwenda ujerumani kutoka katika studio moja ndogo mjini new york. Sasa, matangazo ya VOA, shirika huru linalofadhiliwa na serikali, yanafikia zaidi ya watu millioni 280 kwa wiki kote duniani katika lugha zaidi ya 40.

Habari zake, zikizungumzia matukio ya ndani ya Marekani na nchi nyingine duniani, zinapatikana kwa njia ya mtandao, televisheni na radio. Matangazo ya VOA yanarushwa na radio shirika zaidi ya 2,500.

Katika matangazo yake ya kwanza mwaka 1942, kiasi cha wiki saba baada ya marekani kuingia katika vita kuu ya pili duniani, wasikilizaji kwanza walisikia wimbo wa kizalendo wa marekani “the battle hymn of the republic.” Na kufuatiwa na mtangazaji William Harlan Hale aliyesema, “Tunawaletea Sauti kutoka Amerika, na kila siku kuanzia sasa tutazungumza na nyinyi kuhusu Amerika na vita (hii). Habari zinaweza kuwa nzuri kwetu. Habari zinaweza kuwa mbaya. Lakini tutawaambia ukweli.”

VOA ni sehemu ya USAGM, idara ya serikali inayosimamia matangazo yote ya kimataifa yasiyo ya kijeshi.

Waandishi wa VOA wanaandaa habari chungu nzima kila siku bila kuingiliwa na serikali ya Marekani.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG