Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 15, 2024 Local time: 09:11

Saudi Arabia yamwachia huru Prince Talal


Hoteli ya Prince Talal, Ritz-Carlton huko Riyadh ambako alikuwa anashikiliwa.
Hoteli ya Prince Talal, Ritz-Carlton huko Riyadh ambako alikuwa anashikiliwa.

Kwa zaidi ya siku 80 alikuwa amewekwa kizuizini, bila ya kuwa na mawasiliano, katika mji mkuu wa Mamlaka ya Saudi Arabia wakati wasiwasi ukienea kati ya ndugu na washirika wake wa kibiashara.

Gazeti la New York Times la Marekani limeripotikuwa Jumamosi, Prince Alwaleed bin Talal, mwekezaji mashuhuri wa Saudi Arabia kuliko yoyote na mmoja wa watu matajiri sana ulimwenguni, aliibuka, akionyeshwa katika video iliyorikodiwa akitembelea hoteli yake ya kifahari the Ritz-Carlton hotel huko Riyadh, ambayo amesema yalikuwa makazi yake kwa miezi kadhaa iliopita.

Katika mahojiano yake na shirika la habari la Reuters Prince Talal alisema: ” Niko vizuri kabisa kwani niko katika nchi yangu. Katika mji wangu. Hivyo najihisi niko nyumbani. Hakuna tatizo lolote kabisa. Kila kitu kiko sawa sawa.

Baada ya masaa machache Prince Talal aliachiwa huru na kurejea katika kasri yake huko Riyadh kwa mujibu wa watu wa karibu wa familia yake ambao waliomba wasitajwe majina kwa kuwa kuachiwa huku hakukutangazwa rasmi na serikali ya Saudi Arabia.

XS
SM
MD
LG