Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Agosti 14, 2022 Local time: 22:40

Nini cha kutarajia katika hotuba ya Trump?


Rais Donald Trump

Wakati atapotowa hotuba yake ya hali ya taifa la Marekani Jumanne usiku, Rais Donald Trump atazungumzia “kuweka wazi juu ya marafiki na maadui” wa Marekani na juhudi zake za “kuwashinda magaidi duniani,” Afisa wa ngazi ya juu wa serikali amesema Jumamosi.

Ikulu ya White House haijaeleza kwa uwazi lakini maafisa wamethibitisha kuwa Suala la uwezo wa Korea Kaskazini kutengeneza kombora lenye kichwa cha nyuklia ambalo litaweza kuipiga Marekani linatarajiwa kuwepo katika hotuba yake.

Hotuba hiyo ya kila mwaka inayotolewa na marais wa Marekani kwa mabunge ya Marekani huwa inajikita zaidi katika masuala ya kitaifa. Hotuba ya Trump haitokuwa tofauti. Pia itakuwa ni muhimu kwa wasikilizaji ulimwenguni kote, kwa kuwa atazungumzia usalama wa taifa, biashara na uhamiaji.

Trump pia “atasisitiza kuwepo usawa na namna ya kushirikiana kibiashara,” kwa mujibu wa afisa huyo, ambaye aliwapa muhtasari wa hotuba hiyo akiwataka wasimtambulishe. Hatua zilizochukuliwa hivi karibuni na Marekani dhidi ya namna China inavyofanya biashara pia huenda zikaelezwa.

Wakati siku zikikaribia kutolewa hotuba hiyo, ambayo inatarajiwa kudumu kwa saa moja, ikulu ya White House imeainisha mapendekezo ya Trump juu ya mabadiliko ya uhamiaji, na maafisa wanasema kuwa rais, katika hotuba yake ya Hali ya Taifa, atawataka Wabunge wa Congress kupitisha mabadiliko hayo pamoja na kuwa hapo awali wabunge wengi hawakufurahishwa na mabadiliko hayo.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG