Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 15:01

Naibu mrithi wa ufalme Saudi Arabia akutana na Trump


Mohammed bin Salman
Mohammed bin Salman

Naibu mrithi wa kiti cha ufalme Saudi Arabia Mohammed bin Salman ameondoka Saudi Arabia Jumatatu kuelekea Marekani na atafanya mazungumzo na Rais Donald Trump, ofisi ya mfalme imesema katika taarifa iliyochapishwa na shirika la habari la taifa SPA.

Utakuwa ni mkutano wa kwanza kati ya mtoto mwenye madaraka makubwa wa Mfalme wa Saudi Salman bin Abdulaziz, ambaye anasimamia mpango wa mageuzi ya kiuchumi ya Saudi, na rais wa Marekani tangu Trump alipochukuwa madaraka Januari.

Taarifa hiyo imesema kuwa wakati atapofanya mazungumzo na Trump na maafisa wengine wa Marekani, anategemewa kuzungumzia jinsi ya kuimarisha mahusiano kati ya nchi hizo mbili na kupitia tena masuala yenye maslahi ya pande mbili huko mashariki ya kati.

Imesema kuwa ziara hiyo ya kikazi itaanza Alhamisi lakini hakutoa maelezo zaidi.

Mfalme Salman, mtawala wa nchi inayoongoza katika kuuza mafuta ulimwenguni, hivi sasa yuko Japan, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya mwezi mmoja kujenga mahusiano na nchi zinazo ongoza kwa kasi uagizaji mafuta ghafi na kupanua nafasi za uwekezaji, ikiwemo kuuza hisa katika kampuni kubwa ya mafuta ya Saudi Aramco.

Trump amezungumza kwa simu na Salman mara baaada ya kuchukua madaraka Januari na amekubali kusaidia ujenzi wa maeneo salama kwa ajili ya wakimbizi huko Syria na Yemen, kwa mujibu wa taarifa ya White House.

Kabla ya kuondoka kwenda Marekani, Mfalme Salman alikutana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Citigroup Michael Corbot Riyadh Jumapili kuzungumzia fursa za uwekezaji katika nchi yake na duniani, SPA imeripoti.

XS
SM
MD
LG