Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Januari 31, 2023 Local time: 13:28

Rwanda italazimika kutotegemea ngano inayouzwa na Russia


FILE - Wakulma wakivuna ngano kwa mashine kusini mwa mkoa wa Stavropol, Russia, July 9, 2014. (Photo by DANIL SEMYONOV / AFP)

Serikali ya Rwanda imeripoti inafanya mipango ya kutafuta sehemu mbadala ambako inaweza kuagiza ngano kutokana na uhaba wa bidhaa hiyo ambayo inaagizwa kwa kiwango kikubwa kutoka Russia.

Katika kikao na waandishi wa habari mjini Kigali, Waziri Mkuu Edouard Ngirente amesema Rwanda inajitayarisha na namna ya kukabiliana na mgogoro wa kiuchumi kutokana na uvamizi wa Russia nchini Ukraine, ikiwemo ongezeko kubwa la bei ya mafuta.

Amesema kwamba asilimia 64 ya ngano inayotumika Rwanda, inatoka Russia na husafirishwa kupitia Tanzania.

Amesema kwamba serikali ya Rwanda inatafuta sehemu mbadala inapoweza kuagiza ngano.

Ngirente ameongezea kuwa wataanza kuhisi makali ya mgogoro huo kupitia kwa kupanda kwa bei ya mafuta baada ya mwezi mmoja hivi, na kwamba kwa sasa, wanatumia akiba ya mafuta walioagiza miezi miwili iliyopita.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG