Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 05, 2023 Local time: 18:01

ICC yamwachia huru William Ruto


 Makamu Rais wa Kenya William Ruto
Makamu Rais wa Kenya William Ruto

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC) imeamua Makamu wa Rais wa Kenya William Ruto hana kesi ya kujibu kuhusiana na mashtaka ya uhalifu dhidi ya binadamu yaliyokuwa yanamkabili.

Aidha, imeamua pia kwamba mwanahabari Joshua arap Sang, aliyeshtakiwa pamoja na Bw Ruto, naye pia hana kesi ya kujibu.

Bw Ruto alikabiliwa na mashtaka ya mauaji, kuhamisha watu kwa lazima na mateso yaliyotekelezwa wakati wa vita vya baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007.

Alikana mashtaka hayo na mawakili wake walitaka kesi hiyo itupiliwe mbali kutokana na ukosefu wa ushahidi. Watu takriban 1,200 waliuawa wakati wa mapigano hayo.

Majaji wamesema upande wa mashtaka haukutoa ushahidi wa kutosha kuthibitisha madai dhidi ya Bw Ruto na Bw Sang.

XS
SM
MD
LG