Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 15:28

Daktari Oduor atoa ripoti ya kilichosababisha kifo cha Msando


Marehemu Chris Msando
Marehemu Chris Msando

Uchunguzi uliofanywa kwenye mwili wa aliyekuwa Meneja wa ICT katika Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) Chris Msando umeonyesha kilichosababisha kifo chake.

Alikuwa amenyongwa, uchunguzi wa upasuaji uliofanyika Jumatano katika Nyumba ya Matayarisho ya Maziko mjini Nairobi umedhihirisha hilo.

“Alikufa kutokana na kukabwa na pia kuchomwa na kitu chenye ncha kali katika mkono wake wa kulia lakini sehemu zilizobakia katika mwili wake zilikuwa hazijaathirika na kitu chochote,” amesema Mtaalam Mpasuaji wa Serikali Johansen Oduor, akiwa kati ya wataalamu waupasuaji wengine, aliyesimamia upasuaji wa uchunguzi huo.

Uchunguzi huo ulishuhudiwa pia na wapasuaji wataalamu wawili, moja kutoka serikalini na mwengine aliyekuwa ameteuliwa na familia ya marehemu.

Wakati wakisubiri matokeo ya uchunguzi huo, familia ya marehemu imewataka watu Kenya kwenye mitandao ya kijamii wapime kuwa familia iko katika maombolezi na waache kuposti habari zenye uchochezi.

“Tunawaomba watu hao wawajibike katika mitandao hiyo ya kijamii na kuwa baadhi ya vitu vinavyowekwa katika mitandao hiyo ni uongo,” amesema Peter Msando.

XS
SM
MD
LG