Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 09, 2024 Local time: 03:48

Reuters, AFP wasema shambulizi lilifanywa na mizinga ya Israel dhidi ya waandishi


Kamera ya mwandishi Issam Abdallah katika shambulizi lililofanywa na mizinga ya Israel.
Kamera ya mwandishi Issam Abdallah katika shambulizi lililofanywa na mizinga ya Israel.

Vyombo vya habari vya  Reuters na Agence France-Presse vimechapisha uchunguzi kuhusu shambulio la Oktoba kusini mwa Lebanon ambalo lilimuua mwandishi wa habari na kuwajeruhi wengine sita, wakisema matokeo yao yanaonyesha kuwa wanahabari hao walipigwa na mizinga ya Israel.

Kila shirika la habari lilifanya uchunguzi na wataalam wa nje kukagua rekodi za video, picha za satelaiti, ushuhuda wa mashahidi na vipande vya silaha, na kuhitimisha kuwa shambulizi hilo lilikuwa la mizinga 120, mizinga inayotumiwa na jeshi la Israeli pekee.

Shambulio hilo lilitokea Oktoba 13 wakati waandishi hao walipokusanyika karibu na kijiji cha mpakani cha Lebanon cha Alma al-Chaab ili kurekodi video ya maeneo ya karibu ambapo kumekuwa na mapigano ya mpaka kati ya jeshi la Israel na wapiganaji wa Palestina.

Reuters na AFP zilisema waandishi hao walitambulika wazi kuwa ni wanaandishi wa habari wakiwa wamevalia jaketi na Kofia .

Shambulizi la awali lilipiga kundi hilo, likifuatiwa haraka kwa sekunde, mashirika ya habari yalisema. Mwandishi wa habari wa Reuters, Issam Abdallah aliuawa, huku wenzake wawili wa Reuters na mwandishi wa habari wa AFP wakiwa miongoni mwa waliojeruhiwa.

Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la Reuters na AFP.

Forum

XS
SM
MD
LG