Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 08, 2024 Local time: 14:53

Guterres aendelea kusisitiza kusimamishwa mapigano Gaza


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres,  Jumanne amerejea wito wake wa kusitisha mapigano kwa ajili ya juhudi za kibinadamu katika Ukanda wa Gaza, akionya kwamba utulivu wa umma unaweza kusambaratika kabisa hivi karibuni, na mfumo wa kibinadamu huko uko kwenye hatari kubwa ya kuporomoka.

Guterres amesema wakati wa mashambulizi ya mara kwa mara ya Israeli, na bila makazi au mahitaji muhimu ya kuishi, anatarajia hali ya utulivu kwa umma itavunjika hivi karibuni kutokana na hali ya kukata tamaa.

Ameongeza kusema kwamba hata msaada mdogo wa kibinadamu hauta wezekana.

Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa aliliandikia baraza la usalama kulingana na kifungu cha 99 cha mkataba machache kuyaleta mataifa 15 yenye nguvu kutambua jambo linalo tishia amani na usalama wa kimataifa.

Forum

XS
SM
MD
LG