Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 09, 2024 Local time: 04:23

Mwendesha mashitaka wa ICC ainyooshea kidole Israel


Mwendesha mashitaka wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu – ICC, Jumapili ametoa mwito kwa Israel, kuheshimu sheria za kimataifa za kivita.

Pia amesema anaongeza kasi ya uchunguzi wake wa ukiukwaji wa haki unaofanywa na walowezi dhidi ya Wapalestina huko Ukingo wa Magharibi.

Mwendesha mashitaka wa ICC, Karim Khan, amesema kwamba ndani ya Gaza, hakuna hoja ya msingi ya kwa nini madaktari wanafanya shughuli zao bila ya taa, na watoto kufanyiwa operesheni bila dawa ya kuwaondoa fahamu ili kupunguza maumivu.

Amesema wasaa huu amekuwa muwazi kabisa wa kufuatwa kwa sheria, na kama Israel haifuati sasa basi isilaumu baadaye.

Israel, imeapa kulitokomeza kundi la Hamas, na kusema lengo lake ndani ya Gaza, ni kusambaratisha malengo yake yote ya kundi hilo, huku ikiwasihi raia kuondoka katika maeneo hayo.

Khan pia ameitaka Hamas, ambayo Marekani imelitangaza kuwa kundi la kigaidi liheshimu sheria.

Forum

XS
SM
MD
LG