Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 28, 2023 Local time: 22:32

Ramaphosa atangaza mafuriko yanayoendelea nchini Afrika Kusini kuwa ni janga la kitaifa


FILE PHOTO: South Africa's Ramaphosa delivers state of the nation address

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ametangaza hali ya maafa kitaifa ili kuwezesha majibu kutokana na mafuriko yaliyosambaa yameathiri  majimbo saba kati ya tisa ya nchi hiyo.

Majimbo ya Mpumalanga na Eastern Cape yameathiriwa zaidi na mafuriko hayo, ambayo yamesababishwa na mvua kubwa zilizonyesha ikiwa ni matokeo ya hali ya hewa ya La Nina, kulingana na taarifa kutoka ofisi ya rais, Jumatatu.

Majimbo mengine yaliyokumbwa na mafuriko ni Gauteng, KwaZulu-Natal, Limpopo, Northern Cape, na North West, na kulifanya tangazo la janga la kitaifa kuipa serikali mamlaka ya ziada, ikiwa pamoja na ununuzi, usambazaji wa bidhaa na huduma na kuipa serikali uwezo wa kufanya maamuzi bila kufuata masharti yaliyowekwa kwa mujibu wa sheria ya sasa.

Jeshi la polisi na kikosi cha ulinzi huenda vitapelekwa kutoa misaada katika maeneo yaliathiriwa, ilisema taarifa hiyo kutoka.

Mafuriko hayo yamesababisha athari mbali mbali, kuanzia nyumba na magari kukumbwa namafuriko ikiwa ni pamoja na kusababisha “uharibifu wa miundo mbinu muhimu” taarifa hiyo ilieleza.

Wiki iliyopita rais Ramaphosa alitangaza hali ya maafa ya kitaifa kutokana na tatizo la kila siku la kukatika kwa umeme, tatizo ambalo linadumaza biashara.

-Chanzo cha habari hii inatoka shirika la habari la Reuters

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG