Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 13:51

Meli ya kijeshi ya Russia yatia nanga Cape Town kabla ya mazoezi ya pamoja na Afrika Kusini na China


Meli ya kijeshi ya Russia, "Admiral Gorshkov"
Meli ya kijeshi ya Russia, "Admiral Gorshkov"

Meli ya kijeshi ya Russia ilitia nanga katika Bahari ya Cape Town Jumatatu kabla ya mazoezi ya pamoja yenye utata na Afrika Kusini na China, yanayojiri wakati Moscow inakaribia kuadhimisha mwaka mmoja tangu uvamizi wake unaoendelea nchini Ukraine.

Ubalozi mdogo wa Russia mjini Cape Town umechapisha kwenye ukurasa wake wa Twitter picha ya meli hiyo “Admiral Gorshkov”, ikiwa bandarini, ukisema kwamba ilikuwa ikielekea Durban ambako itashiriki katika mazoezi ya pamoja”.

Mazoezi hayo yaliyopewa jina la “Mosi”, ikimaanisha moshi katika lugha ya Afrika Kusini ya Kitswana, yamepangwa kufanyika Februari 17 hadi Februari 27 nje ya miji ya bandari ya Durban na Richards Bay.

Yatakwenda sambamba na kumbukumbu ya mwaka wa kwanza wa uvamizi wa Russia nchini Ukraine tarehe 24 Februari.

Zaidi ya wanajeshi 350 wa Afrika Kusini watashiriki mazoezi hayo “kwa lengo la kubadilishana ujuzi na maarifa” na Russia na China, jeshi la Afrika Kusini lilisema mwezi uliopita, ikiwa ni mazoezi ya pili kama hayo kati ya vikosi vitatu vya majini.

Mfumo wa makombora wa Zircon kwenye meli ya kijeshi ya Russia “ni wa aina yake”, Rais Vladimir Putin alinukuliwa akisema mwezi uliopita wakati wa uzinduzi wa meli ya kivita kwa ajili ya mafunzo katika bahari ya Atlantiki na Hindi na bahari ya Mediterania.

XS
SM
MD
LG