Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 14, 2024 Local time: 09:22

Ligi ya mabingwa Afrika: Timu zilizocheza nyumbani zaanza vyema


Mashabiki wa Wydad AC wakiiunga mkono timu yao wakati wa mechi ya fainali ya soka ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Wydad Athletic Club ya Morocco na Al Ahly SC ya Misri.May 30, 2022. AP
Mashabiki wa Wydad AC wakiiunga mkono timu yao wakati wa mechi ya fainali ya soka ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Wydad Athletic Club ya Morocco na Al Ahly SC ya Misri.May 30, 2022. AP

Timu ya Horoya ilitoka na ushindi muhimu katika michuano ya ligi ya mabingwa Afrika baada ya kuifunga Simba Sports club ya Tanzania kwa bao 1-0 nyumbani Guinea siku ya Jumamosi.

Lakini timu hiyo ilicheza huku mashabiki wao wakiwa roho juu katika robo saa ya mwisho hasa baada ya Ndiaye kukosa penalti iliyookolewa na kipa wa Simba Aishi Manula na huku timu hiyo ikiwazidishia presha.

Ushindi huo unawafanya Horoya kushika nafasi ya pili kwenye kundi D nyuma ya Raja Club Athletic ya Morocco ambao waliwachakaza Vipers SC ya Uganda kwa jumla ya mabao 5-0 kwenye mechi yao ya ufunguzi siku ya Ijumaa.

Wenyeji walipata bao la kuongoza katika baada ya dakika 18 wakati Pape Ndiaye alipoachwa bila ulinzi mkali na kufunga bao kwa kichwa baada ya kona kuchongwa na Amadou Djibo.

Dakika tano baada ya kipindi cha pili kuanza, walipata nafasi nyingine ya dhahabu baada ya kupiga krosi iliyopanguliwa na kumkuta Djibo kwenye posti ya nyuma, lakini hakuweza kulenga lango kwa kichwa akiwa na goli wazi. Kwa upande mwingine, Simba ilipata nafasi baada ya Clatous Chama kupiga mpira wa adhabu lakini kipa aliokoa na kupata kupata kona.

Dakika ya 72, Horoya alipaswa kufunga bao baada ya Joash Onyango kunawa mpira akiwa ndani ya eneo la hatari, lakini Pape Ndiaye alikosa penalti iliyookolewa na Aishi Manula.

Kuanzia hapo, Simba walifanya mashambulizi huku Chama akiupiga mpira nje ya goli dakika ya 75 kabla ya John Bocco aliyetokea benchi kupoiga mpira nje akiwa peke yake na golikipa.

Kipa wa Horoya, Moussa Camara aliokoa vyema zikiwa zimesalia dakika saba kuulinda mpira wa kichwa uliopigwa na Sadio Kanoute kabla ya Bocco kupata nafasi nyingine kuzuiwa ndani ya eneo la hatari.

Juhudi za Simba kupata sare kwenye eneo la adui hazikufua dafu na sasa wanaelekeza nguvu zao wikendi ijayo watakapowakaribisha Raja ya Morocco mjini Dar es Salaam huku Horoya wakisafiri ugenini kuelekea Kampala kumenyana na Vipers ya Uganda.

Mamelodi Sundown yaiangusha Al Hilal

Na katika mchezo mwingine wa kundi timu ya Mamelodi Sundowns, ya Afrika Kusini, ilianza kampeni yake vyema ya kuwania kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ya TotalEnergies CAF kwa ushindi mgumu wa 1-0 dhidi ya Al Hilal ya Sudan iliyokuwa imebaki ba wachezaji kumi mjini Pretoria siku ya Jumamosi.

Bao pekee la Cassius Mailula katika kipindi cha kwanza ndilo lilioipa ushindi vijana wa Afrika Kusini huku Al Hilal wakilazimika kumaliza mechi na wachezaji 10 kufuatia kadi nyekundu.

Beki Altayeb Abaker alitolewa nje kwa kadi nyekundu zikiwa zimesalia dakika nne mchezo huo kumalizika kufuatia kadi ya pili ya njano kwa kitendo chake cha kuzuia mpira uliokuwa ukimpita kwa makusudi kwa mikono.

Mailula alifunga bao la ushindi katika dakika ya 25 ya mechi hiyo alipojibu kwa haraka zaidi kuutumbukiza mpira wavuni kwa karibu na goli baada ya kipa wa Hilal Ali Abdala Abosheren kutema shuti kali kutoka pembeni mwa eneo la hatari na lililopigwa na Neo Maema.

Nafasi nzuri zaidi ya Hilal kusawazisha kabla ya mapumziko ilikuwa dakika ya 28 wakati krosi kutoka upande wa kulia ilipomkuta Mohamed Abdelrahman ndani ya eneo la hatari, lakini nahodha huyo hakuweza kutumia nafasi ya kuweka mpira ndani ya wavu alipopiga kichwa bila kulenga goli.

Katika kipindi cha pili, iligeuka kuwa vita vya utalaam kati ya pande hizo mbili. Sundowns walipata nafasi nzuri huku Mailula nusura afunge bao la pili, lakini juhudi zake zilizuiwa na kipa Abosheren.

Lakini hadi mwisho wa mchezo Mamelodi Sundowns imetoka na pointe zote tatu na ushindi wa bao 1-0.

Esperance ya Tunisia yaanza vyema

Timu ya Esperance ya Tunisia wakiilaza El Merrikh ya Sudan kwa bao 1-0 kwenye Uwanja wa Olympic mjini El-Menzah, na kuanza mechi ya Kundi D ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa ushindi.

Mshambuliaji Mohamed Amine Tougai alifunga bao hilo katika dakika za majeruhi huku washabiki wa Al-Mereikh walipokuwa na matumaini mchezo huo umeisha kwa sare.

Matokeo hayo yanawafanya Esperance wawe katika nafaso ya juu na CR Belouizdad ya Algeria ambao walianza kampeni yao kwa ushindi dhidi ya Zamalek ya Misri mjini Cairo siku ya Ijumaa.

Esperance walijua lazima waanze kwa nguvu katika kile kinachochukuliwa kuwa kundi la kifo kwenye shindano hilo na walipata nafasi ya mapema huku Anice Badri akipiga shuti nje. Ali Bin Ramadhani pia shuti lake lilipaa juu.

Esperance sasa itaelekeza umakini wake kwenye pambano lijalo watakaposafiri ugenini Algeria kumenyana na Belouizdad katika mtanange wa kutafuta atakayekaa kileleni na Merrikh wakiwa nyumbani dhidi ya Zamalek.

XS
SM
MD
LG