Uchunguzi huo umegundua kwamba mkataba uliotolewa kwa kampuni ya Digital Vibes haukuwa sahihi na maafisa wa juu wamefaidika kutokana na baadhi ya pesa zilizolipwa na kampuni hiyo.
Ripoti ya uchunguzi dhidi ya ya kashfa hiyo ilikabidhiwa kwa rais mwezi Julai.
Kumekuwa na mwito uliojirudia ripoti hiyo kutolewa kwa umma.
Katika taarifa iliyotolewa Jumatano ofisi ya rais imesema kwa manufaa ya usawa, pande zote zilizotajwa katika ripoti ya mwisho lazima zijulishwe kabla ya ripoti kutolewa ili wapate nafasi ya kupinga kuchapishwa kwake au kukubali.
Hivi sasa ripoti hiyo imechapishwa kwenye tovuti ya ofisi ya rais. Wiki iliyopita Wizara ya Afya ilitangaza kuondolewa kwa Mkurugenzi Mkuu wa Afya, Sandile Buthelezi dhidi ya suala hilo.