Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Februari 06, 2023 Local time: 10:44

Rais wa madaktari Uganda ashambuliwa na 'majambazi'


Dkt Anthony Ekwaro Obuku

Rais wa Chama cha Madaktari nchini Uganda, Daktari Anthony Ekwaro Obuku, amesema kuwa shambulizi lililofanyika dhidi yake wiki iliyopita haliwezi kumtishia kuacha kupigania maslahi ya madaktari.

“Kwa namna yoyote ile shambulizi hili haliwezi kunishawishi kwamba pengine tubadilishe mbinu [katika kuelezea madhila yetu juu ya maslahi ya madaktari] au [tusitishe mgomo] wote kwa pamoja,” Dkt Obuku ameliambia gazeti la Monitor Jumatano.

Dkt Obuku, ambaye aliongoza madaktari nchini kote kujiunga na mgomo Novemba 2017, wakidai maslahi yao yaboreshwe, alishambuliwa na wanaoshukiwa kuwa ni majambazi wakati akiwa anaingia getini nyumbani kwake eneo la Kitikifumba, Manispaa ya Kira, Jumatano.

Majambazi hao ambao walitoweka na saa yake ya mkononi, pochi yake na simu ya mkononi baada ya kuvunja dirisha lake la gari, pia walisababisha majeraha katika uso wake. Mara moja alipelekwa Case Hospital Kampala.

Dkt Obuku amesema pamoja na kuwa hataki kukubaliana na kushukiwa kuliko elezwa awali kwamba ni shambulizi la kisiasa, lakini bado anawaza vipi majambazi wa kawaida walikuwa wamevalia vizuri sana na wanazungumza Kiingereza fasaha akiliwalinganisha na wale waliomshambulia.

“Walikuwa wamevalia vizuri sana… Kwa hivyo mtu anajiuliza iwapo walikuwa majambazi au mashushu wa serikali… na vipi walijua kuwa mimi siwezi kuzungumza lugha ya Luganda… na kuwa nilikuwa najua Kiingereza,” amesema.

"Uchunguzi wa madaktari unaonyesha kuwa nilipata mpasuko wa mifupa ya usoni [mifupa inayozunguka mdomo na pua na inayoshikilia eneo la jicho, ikiwemo mifupa ya chini ya uso] na eneo la pua; ambayo imepindisha meno yangu na hivi sasa siwezi kula nyama,” amesema.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG