Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:23

Rais wa Ivory Coast atangaza amri ya kutotoka nje


Wapigaji kura wa Abidjan wakisubiri kupokea vitambulisho vya kupiga kura.
Wapigaji kura wa Abidjan wakisubiri kupokea vitambulisho vya kupiga kura.

Rais Laurent Gbagbo wa Ivory Coast ametangaza amri ya kutotoka nje kuanzia Jumamosi hadi Jumatatno, katika lengo la kudumisha utulivu. Lakini uwamuzi unapingwa vikali na upinzani unaosema unakwenda kinyume na sheria.

Rais Gbagbo altoa amri hiyo baada ya watu wanne kuuliwa na polisi mjini Abdijan siku ya Jumamosi, mkesha wa duru ya pili ya uchaguzi wa rais.

Lakini mpinzani wake waziri mkuu wa zamani Alassane Outtara, anasema amri mpya ya kutotoka nje ni haramu na upinzani hauta heshimu amri hiyo. Mvutano huo umesababisha ghasia zaidi na watu watatu wameuwawa katika mapambano na polisi.

Hapo awali Rais Gbabgo alitangaza amri ya kutotoka nje itanza Jumapili usiku baada ya uchaguzi ili kuzuia ghasia na kuepusha uingiliaji kati utaratibu wa kuhesbu kura.

Siku ya Jumamosi mpatanishi wa mzozo wa kisiasa wa Ivory Coast, Rais Blaise Compaore alikua mjini Abidjan kwa mazungumzo na Bw. Gbagbo na Bw. Outtara juu ya sula la amri ya kutotoka nje na masuala mengine muhimu.

XS
SM
MD
LG