Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 23:02

Mbeki akutana na walojitangazia ushindi wa rais Ivory Coast


Jordanian United Nations soldiers stand guard at the entrance to the Golf Hotel in Abidjan, Ivory Coast, 05 Dec 2010
Jordanian United Nations soldiers stand guard at the entrance to the Golf Hotel in Abidjan, Ivory Coast, 05 Dec 2010

Mwakilishi wa Umoja wa Afrika, rais wa zamani wa Afrika Kusini Thabo Mbeki, amekutana na wagombea wawili wa rais wa Ivory Coast ambao walijitangaza kuwa rais wa nchi hiyo mjini Abidjan hapo siku ya Jumapili.

AU inasema ziara ya dharura ya Bw. Mbeki, ina azma ya kupata suluhisho halali na la amani kwa mzozo huo. Mpatanishi huyo wa AU katika vikao tofauti, alikutana na Laurent Gbagbo na Alassane Outtara.

Bw. Mbeki aliwambia waandishi habari kwamba amekwenda huko kusikiliza kila upande ili kufahamu jinisi hali ilivyo. Bw. Outtara amewambia waandishi habari kwamba alimuarifu Bw. Mbeki kwamba yeye ndiye rais wa halali wa nchi na amemtaka Bw. Gbagbo kumkabidhi madaraka.

Laurent Gbagbo alikula kiapo ya kuiongoza nchi siku ya Jumamosi kwa misingi kuwa, baraza la katiba limempa ushindi wa asilimia 51 ya kura. Takriban asilimia kumi ya kura zilibatilishwa kwasababu ya ubadhirifu.

Bw. Ouattara naye alikula kiapo kuchukua madaraka siku hiyo hiyo kwa misingi kuwa, tume ya uchaguzi ilimpa ushindi wa asilimia 54 ya kura. Matokeo hayo yaliidhinishwa na Umoja Mataifa kulingana na mkataba wa amani wa mwaka 2007.

Maafisa waandamizi wa jeshi ambao wanadhibiti eneo la kusini wanamuunga mkono Bw. Gbagbo. Waliokuwa waasi ambao bado wanadhibiti maeneo ya kaskazini wanamuunga mkono Bw. Ouattara.

Madai ya Bw. Ouattara ya kushinda uchaguzi yanaungwa mkono na Jumuia ya Kimataifa.

Bw.Ggbagbo anasema taarifa hizo za kumuunga mkono Ouattara si sawa na uingiliaji wa nje ndio unatishia usalama wa taifa wa Ivory Coast.

XS
SM
MD
LG