Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 07, 2024 Local time: 10:58

Rais wa Indonesia Widodo awanasihi Marekani, China, Russia kuepusha ‘vita vipya’


Rais wa Indonesian Joko Widodo akitoa hotuba yake ya kufunga tafrija ya kumalizika mkutano wa viongozi wa jumuiya ya ASEAN wa 43 huko Jakarta, Indonesia, Septemba 7, 2023. REUTERS/Willy Kurniawan/Pool
Rais wa Indonesian Joko Widodo akitoa hotuba yake ya kufunga tafrija ya kumalizika mkutano wa viongozi wa jumuiya ya ASEAN wa 43 huko Jakarta, Indonesia, Septemba 7, 2023. REUTERS/Willy Kurniawan/Pool

Katikati ya uhasimu mkali wa kisiasa kieneo  kati ya Marekani, China na Russia, Rais wa Indonesia Joko Widodo amewasilisha ujumbe mzito kwa viongozi kupunguza mivutano na kuepusha vita katika eneo hilo.

Akiongea Alhamisi mjini Jakarta wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Asia Mashariki (EAS) unaowaleta pamoja jumuiya ya nchi za Asia Kusini Mashariki (ASEAN) na washirika wake – Marekani, China, Russia, Australia, India, Japan, New Zealand, na Korea Kusini, Widodo alisisitiza umuhimu wa uthabiti katika eneo hilo ili kuendeleza utulivu na mafanikio ya miongo kadhaa iliyopita.

“Kila moja katika ukumbi huu ana jukumu sawa la kutoanzisha mgogoro mpya, kutoanzisha mivutano mipya, kutoanzisha vita vipya,” alisema, akizungumza kwa lugha ya Kiindonesia.

“Wakati huo huo, tunajukumu la kupunguza migogoro mikali, kulainisha masuala yaliyo kwama, kuweka mazingira ya mdahalo, na kusuluhisha tofauti zilizokuwepo.”

Lakini, viongozi wa mataifa matatu yenye nguvu – Rais wa Marekani Joe Biden, Rais wa China Xi Jinping na Rais wa Russia Vladimir Putin – waliamua kutohudhuria mkutano huo, wakipeleka badala yake wawakilishi wao, Makamu wa Rais Kamala Harris, Waziri Mkuu Li Qiang na Waziri wa Mambo ya Nje Sergey Lavrov

Wakati mwenyekiti wa ASEAN anayemaliza muda wake, mapema wiki hii Widodo alitangaza kuwa jumuiya hiyo “imekubaliana kutokuwa wakala wa taifa lolote. Alisisitiza kuwa Asia Kusini Mashariki haitakuwa ni mstari wa mbele wa Vita Baridi vipya – ahadi aliitoa wakati apochukua uongozi wa ASEAN kutoka Cambodia mwaka 2022.

Mwelekeo wa Indonesia katika kukabiliana na siasa za mataifa yenye nguvu haujawahi kubadilika, alisema Aaron Connelly, mtafiti katika Taasisi ya International Institute inayotafiti mikakati.

“Wanaangalia mivutano ya mataifa yenye nguvu kama ndiyo tishio la msingi kwa maslahi ya eneo lote,” aliiambia VOA. “Na wanaona ushindani wenye ni tishio, siyo nchi moja ikianzisha ushindani.”

Forum

XS
SM
MD
LG