Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 19:42

Mkutano wa ASEAN wagubikwa na Mgogoro wa umwagaji damu Myanmar na ongezeko la uchokozi wa China


Viongozi wa jumuiya ya mataifa ya Asia Kusini Mashariki wakutana Jakarta, Indonesia.

Mgogoro wa kisiasa wa  umwagaji damu nchini Myanmar na kuongezeka kwa uchokozi wa China umegubika mkutano wa Jumuiya ya Mataifa ya Asia Kusini Mashariki ulioanza Jumanne katika mji mkuu wa Indonesia, Jakarta.

Rais wa Indonesia Joko Widodo amewaambia viongozi wenzake katika mkutano wa jumuiya ya kikanda yenye nchi wanachama kumi kuwa ya ASEAN “wamekubali kutotumiwa” na taifa lolote lenye nguvu, na kusema wao “lazima wawe manahodha wa meli yao kufanikisha amani.”

ASEAN imekuwa ikijitahidi katika majaribio ya kutafuta suluhu ya mgogoro wa Myanmar, ambao umesababisha vurugu tangu jeshi lilipoipindua serikali iliyochaguliwa kidemokrasia ya kiongozi Aung San Suu Kyi Februari 1, 2021.

Utawala wa kijeshi umekubali maafikiano ya nukta tano” yaliyoandaliwa na Jumuiya ya ASEAN miezi kadhaa baada ya mapinduzi hayo, ikijumuisha kumaliza mara mmoja ghasia, mazungumzo ya amani kufanyika kati ya jeshi na wapinzani na usambazaji wa misaada ya kibinadamu.

Lakini utawala wa kijeshi umeshindwa kutekeleza mpango wa ASEAN, umefanya msako uliosababisha umwagaji damu dhidi ya waandamanaji wanaopinga mapinduzi na mashambulizi ya kikatili ya anga dhidi ya uasi wa kutumia silaha ambao unasaidiwa na makundi kadhaa ya waasi ya kikabila ya vijijini ambayo yamekuwa yakipigana kwa miongo kadhaa kwa ajili ya kupata uhuru zaidi.

Kukwama huku kumepelekea jumuiya ya ASEAN hadhi yake katika baadhi ya duru za kidiplomasia kuonekana kama ni chombo kilichopoteza mwelekeo, na kimewagawa wanachama wake katika mikakati yake. Utawala huo umezuiliwa kuhudhuria mikutano yote ya ngazi ya juu, lakini maafisa kutoka Thailand wamefanya mazungumzo ya ana kwa ana na viongozi wa kijeshi mwezi Julai.

Lakini viongozi hao wamekubaliana Jumanne kuiondoa Myanmar katika uenyekiti wake wa jumuiya ya ASEAN 2026 na kuipa Ufilipino kushika wadhifa huo.

Mkutano wa Jumanne umekuja siku kadhaa baada ya China kuzindua ramani mpya ya bahari inayoonyesha madai yake ya eneo kubwa la bahari ya South China Sea, ikiongeza mivutano na majirani zake wa Asia Kusini Mashariki, ikiwemo wale wenye ushindani juu ya madai ya mipaka hiyo.

Makamu Rais wa Marekani Kamala Harris atahudhuria mkutano wa ASEAN wiki hii kumwakilisha Rais Joe Biden, na pia katika jukwaa pana zaidi la kikanda ambalo litajumuisha China, Russia, India na Japan.

Baadhi ya taarifa katika ripoti hii inatokana na mashirika ya habari ya Reuters, Agence France-Presse.

Forum

XS
SM
MD
LG