Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 01, 2023 Local time: 14:46

Mjadala wa kulinda utalii Marekani waibuka baada ya tukio la Las Vegas


Watu wakitoa rambirambi zao katika eneo lililowekwa kwa ajili ya kuomboleza wahanga wa shambulizi la Las Vegas

Wakati Rais Donald Trump akitembelea Las Vegas, Nevada Jumatano baada ya shambulizi lililouwa watu 58 kuna mjadala umejitokeza kuhusu mkakati wa kuzuia shambulizi kama hilo lisitokee katika jiji lolote ambako biashara ya kitalii ni muhimu.

Rais wa Marekani, Donald Trump ataelekea mjini Las Vegas badaye leo ili kuwafariji wale waliopatwa na maafa kufuatia shambulizi la bunduki lililopelekea watu 58 kupoteza maisha.

Mwaka 2016, Las Vegas iliweza kuchangia bilioni za dola katika kipato cha taifa na ilikuwa ni kivutio cha watalii na watu 40 milioni waliotembelea mji huo.

Rais Trump amemzungumzia mtu huyo aliyefanya shambulizi hilo kuwa ni mtu asiye na uungwana na kusema kwamba mjadala kuhusu kanuni mpya za kudhibiti bunduki usitishwe kwa muda.

Mtu huyo alifyatua risasi kwenye umati wa zaidi ya watu 22,000 waliohudhuria tamasha la muziki wa “Country” siku ya Jumapili usiku kabla ya kujiuwa mwenyewe wakati polisi wakimkaribia.

Wakati huo huo wapelelezi wakiendelea kukusanya taarifa za kutambua sababu ya mtu mwenye bunduki kushambulia umma wa watu waliokuwa katika tamasha la muziki.

Mshambuliaji huyo alifanya kitendo hicho cha kinyama kutoka katika chumba chake cha hoteli, na kuua watu 58 na baadaye kujiua mwenyewe.

Pia vyombo vya usalama vimeripoti kuwa watu takriban 527 walijeruhiwa katika tukio hilo.

Mamalaka zimemtaja mtu aliyeshambulia kuwa ni Stephen Paddock mwenye umri wa miaka 64, ambapo pia zimesema tukio hilo la kufyatua risasi lilichukuwa takriban dakika 9 na 11 kutoka chumbani mwake ghorofa ya 32 katika hoteli mjini Las Vegas, Nevada.

XS
SM
MD
LG