Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 12:03

Polisi Marekani bado wanachunguza chanzo cha shambulizi la Las Vegas


Eneo lilipotokea shambulizi la Las Vegas Oct. 3, 2017.
Eneo lilipotokea shambulizi la Las Vegas Oct. 3, 2017.

Sherif wa Las Vegas katika jimbo la Nevada nchini Marekani Joseph Lombordo alisema anaamini kabisa wachunguzi watagundua sababu zilizopelekea mauaji mabaya ya umma katika historia ya Marekani.

Wachunguzi bado hawafahamu kwa nini Stephen Paddock mwenye miaka 64 mtu ambaye alikuwa hana matatizo ya fedha na hakuwa na rekodi ya uhalifu au kujihusisha na masuala ya kisiasa au kidini alifyatua risasi kwenye tamasha la muziki wa Country siku ya Jumapili usiku na kuuwa watu 59 na kuwajeruhi 527.

Polisi wakiwa eneo la tukio Las Vegas Oct. 2, 2017.
Polisi wakiwa eneo la tukio Las Vegas Oct. 2, 2017.

Lombordo alisema Jumanne kwenye mkutano na waandishi wa habari kwamba tukio hilo la mauaji kwa hakika lilikuwa limepangwa. Alisema ana uhakika kabisa kuwa Paddock alifanya tathmini ya kila kitu alichokifanya. Hatuwezi hata kufuta uwezekano wa ugonjwa wa akili au aina fulani ya matatizo ya ubongo japokuwa hakuna ushahidi wa jambo hilo pia ofisa wa usalama wa ndani alisema Jumanne.

Sherif alitoa maelezo machache juu ya kile wachunguzi walichogundua lakini alisema kuwa Paddock alifyatua risasi kutoka ghorofa ya 32 ya hoteli ya Mandalay Bay kwa dakika tisa kabla ya kujiuwa mwenyewe. Alisema maafisa wa serikali kuu kutoka Alcohol, Tabacco na Firearms wanachunguza kuona kama Paddock alitumia kifaa kijulikanacho kitaalamu Bump Stock ambacho kinabadilisha msukumo wa risasi hivyo mtumiaji anaweza kufyatua risasi nyingi kwa haraka zaidi.

XS
SM
MD
LG