Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 23:13

Rais Nyusi hawezi kushtakiwa nchini Uingereza- Mahakama Kuu


Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi

Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi hawezi kushtakiwa nchini Uingereza kwa madai ya kukubali malipo kinyume cha sheria.

Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi hawezi kushtakiwa nchini Uingereza kwa madai ya kukubali malipo kinyume cha sheria.

Malipo hayo ni kuhusiana na kesi ya nchi hiyo dhidi ya benki ya Credit Suisse, na wengine kuhusu kashfa inayojulikana kama "tuna bond" ya dola bilioni 2, Mahakama Kuu ya London iliamua Jumatatu.

Kesi ya sakata ya tuna Bond, ambayo pia imepewa jina la "deni lililofichwa" imepelekea uchunguzi wa jinai kutoka Maputo hadi New York, pamoja na msururu wa kesi zinazouwiana mjini London zinazohusisha taasisi ya Credit Suisse, kampuni ya ujenzi wa meli ya Privinvest, mmiliki wake Iskandar Safa, na wengine wengi.

Privinvest na Safa walijaribu kumuingiza Rais Nyusi kwenye kesi hiyo, wakisema kwamba anapaswa kuchangia fidia yoyote ambayo wanaweza kuagizwa kulipa ikiwa watapatikana na hatia nchini Msumbiji, lakini Mahakama Kuu iliamua Jumatatu kwamba Nyusi ana haki ya kupata kinga ya serikali.

Forum

XS
SM
MD
LG