Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 03, 2024 Local time: 15:39

Madaktari Msumbiji waidhinisha mgomo mpya wa siku 21


Rais wa Msumbiji, Filipe Nyusi
Rais wa Msumbiji, Filipe Nyusi

Madaktari nchini Msumbiji wameidhinisha mgomo mpya Agosti  20 kwa siku 21, ikiwa ni wa tatu mfululizo tangu Julai 10.

Madaktari Wamemuomba rais Filipe Nyusi kumaliza mzozo uliopo ambao unadhoofisha mahospitali.

“Tumeamua kuongeza muda wa mgomo kwa siku 21 kama ilivyokuwa hapo kabla, kwa kupunguza huduma kwa kiwango cha kati ili watu wasitaabike zaidi,” alitangaza hayo rais wa jumuiya ya madaktari msumbiji, Milton Tatia mwishoni mwa Mkutano mkuu huko Maputo.

Mkutano mkuu uliofanyika Jumapili na ulihudhuriwa na dazeni za madaktari ulikuwa na agenda yake ya kuamua kama kuongeza muda wa mgomo ambao ni kwa ajili ya kupinga kupunguzwa mishahara, ikiwa ni sehemu ya maombi ya kiwango kipya cha mishahara ya watumishi wa umma, na ukosefu wa malipo ya ziada ya mishahara baada ya muda wa kazi pamoja na kutetea huduma za afya kitaifa na hadhi ya madaktari.

Kiongozi huyo wa chama cha madaktari aliongeza kusema kuwa tangu kuanza mgomo Julai 10, kumeshuhudiwa aina mbalimbali za vitisho ikiwa ni pamoja na vitisho dhidi ya watu kutokuwepo kazini au kukatwa mishahara na hata kusitishwa kwa kandarasi za wafanyakazi.

Habari hii inatokana na vyombo vya habari vya Msumbiji.

Forum

XS
SM
MD
LG