Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 21, 2024 Local time: 20:25

Rais mpya wa Baraza Kuu la UN afungua kikao cha 75


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres

Kikao cha 75 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) kimefunguliwa rasmi Jumanne na rais mpya wa baraza hilo, Volkan Bozkir.

Wakuu wa nchi na serikali kutoka mataifa wanachama 193 watahutubia kwa njia ya video, kauli mbiu ya mwaka huu ni ‘Hali ya Baadaye Tunayoitaka: Kuthibitisha Kujitolea Kwa Pamoja kwa Nia ya Dhati Kwa Kila Upande.’

Katika matamshi yake ya ufunguzi, Bozkir amesema ni heshima kubwa yeye kuwa mwenyekiti wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na kuelezea shukrani zake kwa mataifa wanachama kwa imani yao kwake.

Hatimaye katika hotuba yake, Bozkir ameyataka mataifa wanachama wa UN kuendeleza ushirikiano wa pamoja, akisema : “Ni wajibu wetu kuimarisha imani ya watu katika ushirikiano wa pamoja na taasisi za kimataifa, huku Umoja wa Mataifa ukiwa katikati. Tunahitaji kuendelea kuwa wakweli, wawazi na mjadala wenye matokeo chanya khusu kitu gani kimekosewa katika juhudi zetu za kudhibiti virusi na nini tufanye ili kuepuka hali kama hii katika siku za usoni. Pia tunahitaji kuhoji na kuuliza maswali kuhusu chanjo ya Covid 19 ambayo itaweza kugaiwa kwa haki na usawa. Hili siyo tu swala la afya na uchumi, lakini ni maadili kwa njia ya kina zaidi.”

Naye Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, katika matamshi yake ya ufunguzi, alimpongeza Bozkir kwa jukumu lake jipya na kuahidi jumps msaada kamili.

"Mwaka huu utakuwa ni muhimu sana katika maisha ya taasisi hii ya dunia. Umoja wa Mataifa lazima uendelee kujibu haraka matokeo ya Covid 19 kwa kuimarisha mifumo ya afya na kusaidia maendeleo na ugawaji wa sawa wa matibabu na chanjo. Pia lazima tutayarishe kujenga mpango madhubuti wa kujifufua, kulingana na ajenga ya mwaka 2030 ya malengo ya maendeleo endelevu na mkataba wa Paris kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa," amesema Katibu Mkuu.

Wakati wote huo, Baraza Kuu litaendelea na kazi zako zote katika changamoto za ulimwengu inazokabiliana nazo: amani na usalama, usalimishaji wa silaha, haki za binadamu, usawa wa jinsia na maendeleo endelevu amesema Guterres.

Guterres ameongeza kusema : "Wakati tukiadhimisha miaka 75 ya Umoja wa Mataifa, ni dhahiri kwamba dunia ina matarajio makubwa sana kutoka kwetu, kama uwanja mkuu kwa ushirikiano pamoja na uhusiano kulingana na mfumo wa kimataifa. Msisitizo wenu ni kuitekeleza ajenda ya Baraza Kuu na kuleta uwiano wa nguzo tatu za kazi yetu katika kuleta mafanikio ya msingi lazima tusaidia katika kufikia matarajio hayo."

Bozkir, alichukuwa hatamu za uongozi wa taasisi hiyo ya dunia huku kukiwa na janga, na kuamua kuchanganya kauli mbiu ya maadhimisho ya 75 ya Umoja wa Mataifa na haja ya kupambana kwa nguvu zote na Covid-19, wakati ambapo kauli mbiu ya kikao cha 75 cha baraza kuu kinaeleza wazi “Hali ya Baadaye Tunayoitaka, Umoja wa Mataifa Tunaouhitaji: Kuthibitisha Kujitolea Kwa Pamoja Kwa Nia Ya Dhati Kwa Kila Upande na Kukabiliana na Covid 19 Kupitia Hatua Zenye Ufanisi.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Harrison Kamau, Washington DC

XS
SM
MD
LG