Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Agosti 19, 2022 Local time: 15:17

Rais Lula atinga jela kwa kashfa ya rushwa


Rais Lula da Silva

Rais mstaafu wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva amehukumiwa kwenda jela kwa takriban miaka 10 siku ya Jumatano kwa sababu ya kupokea rushwa.

Lula ambaye alitoka katika familia ya kimaskini na kuibuka kidedea katika uchaguzi wa urais na baadae kuwa mmoja wa marais mashuhuri sana wa Brazil.

Lula alipata umaarufu mkubwa kutoka katika jumuiya ya kimataifa kwa sababu ya sera zake zilizojikita kuboresha maisha ya watu wanyonge Brazil.

Lakini vyanzo vya habari nchini Brazil vimesema kuwa umaarufu huo umegeuka baada ya kukutwa na hatia ya kukubali rushwa ya zaidi ya dola milioni moja kwa ajili ya nyumba yake binafsi ambapo pesa hizo zingetumika kuikarabati.

Kampuni ambayo inahusishwa na kutoa hongo hiyo ni kampuni ya ujenzi ya Ki Brazil, iitwayo kwa kifupi OAS.

Maamuzi ya kesi yamekuja wakati Lula akiwa tayari amejipanga kuingia katika kinyang’anyiro cha Kugombea nafasi ya urais mwakani, ambaye alikuwa na nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG