Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 06, 2024 Local time: 01:12

Gbagbo atangaza amri ya kutotoka nje Abidjan


Vurugu katika wilaya ya Abobo.
Vurugu katika wilaya ya Abobo.

Kiongozi wa Ivory Coast aliyekataa kuachia madaraka Laurent Gbagbo ameweka marufuku katika katika mtaa mmoja wa Abidjan ambapo mapigano makali yalitokea katika siku za karibuni.

Mkuu wa majeshi Phillipe Mangou ambaye anamuunga mkono Bw. Gbagbo alitangaza Jumatano usiku kwamba wilaya ya Abobo itakuwa chini ya amri ya kutotoka nje kuanzia saa moja usiku mpaka saa kumi na mbili asubuhi hadi siku ya Jumamosi asubuhi. Mangou alidai kwamba majeshi ya usalama yako tayari kwa maneno yake "kujibu mashambulizi".

Abobo ni ngome ya mpinzani wa Bw. Gbagbo Alassane Outtara. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki Moon ameonyesha kwa maneno yake wasi wasi mkubwa juu ya mambo yanayoendelea Abobo na kusema kwamba kuna ripoti za majeshi yanayomtii Bw. Gbagbo kuwa yanajaribu kutumia marufuku hayo kulazimisha walinda amani kuondoka eneo hilo.

Wizara ya mambo ya ndani ya Bw. Gbagbo ilisema Polisi wapatao sita waliuwawa katika eneo hilo jumatano na mashahidi wanasema raia mmoja pia aliuwawa na magari kadhaa ya polisi yalichomwa moto wakati wa mapambano makali ya alfajiri.

XS
SM
MD
LG