Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 21, 2024 Local time: 05:26

EU kuweka vikwazo kwa Gbagbo

Wanajeshi wa Umoja wa Mataifa wakifanya doria mjini Abidjan, Ivory Coast, 12 Dec 2010
Wanajeshi wa Umoja wa Mataifa wakifanya doria mjini Abidjan, Ivory Coast, 12 Dec 2010

Umoja wa ulaya inasema itamuwekea vikwazo rais asiyekubalika wa Ivory Coast Laurent Gbagbo, ambaye anakataa kukabidhi madaraka baada ya kushindwa uchaguzi wa mwezi uliopita.

Umoja wa ulaya inasema itamuwekea vikwazo rais asiyekubalika wa Ivory Coast Laurent Gbagbo, ambaye anakataa kukabidhi madaraka baada ya kushindwa uchaguzi wa mwezi uliopita.

Msemaji wa Umoja wa ulaya alisema Jumatatu bwana Gbagbo na mke wake ni miongoni mwa raia 19 wa Ivory Coast walio katika orodha ya watu wanaokabiliwa na vikwazo. Bwana Gbagbo anakaidi wito wa kukabidhi madaraka kwa Alassane Ouattara, anayetambulika kimataifa kama mshindi katika uchaguzi wa rais uliofanyika nchini humo.

Huku matatizo ya kisiasa yakiendelea Umoja wa Mataifa inaripoti wimbi la mauaji na utekaji nyara nchini Ivory Coast. Kamishna mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulika na masuala ya haki za binadamu, Navi Pillay, alitoa taarifa Jumapili akisema zaidi ya watu 50 wameuwawa na zaidi ya watu 200 walijeruhiwa tangu Alhamisi.

Pillay alisema kuna ushahidi zaidi kuhusu ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu nchini humo. Tume ya Umoja wa Mataifa inasema imepokea mamia ya ripoti za watu kutekwa nyara kutoka majumbani mwao na watu wenye silaha waliovalia sare za kijeshi.

Mapambano ya madaraka yamepelekea wasi wasi wa kurejea tena kwa mapigano nchini Ivory Coast ingawaje maafisa wa pande zote wanasema wanataka kuepuka vita.

XS
SM
MD
LG