Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 08:06

Rais Buhari asikitishwa na unyanyasaji uliofanywa kwa raia wa Nigeria


Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari (Photo by JOHANNA GERON / POOL / AFP)
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari (Photo by JOHANNA GERON / POOL / AFP)

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari ameelezea kutoridhishwa kwake na matukio yaliyoripotiwa ya unyanyasaji wa baadhi ya raia wa Nigeria wanaojaribu kuondoka Ukraine baada ya Russia kuivamia nchi hiyo.

Wanigeria 4,000 bado wamekwama Ukraine. Katika taarifa yake kwenye mtandao wa Twitter ofisi ya rais imesema maafisa wa polisi na usalama wa Ukraine wameripotiwa kuwakatalia wanigeria kupanda mabasi na treni kuelekea kwenye mpaka wa Ukraine na Poland.

Kundi moja la wanafunzi wa Nigeria ambalo limekatawalia mara kadhaa kuingia Poland limesema halikuwa na chaguo lakini kurejea tena Ukraine na kujaribu kuondoka nchini kupitia mpaka wa hungary, taarifa imesema.

Ofisi ya Buhari imesema raia wote wa kigeni wanaojaribu kuvuka mpaka wa Poland lazima wahudumiwe kwa kufuata utu na bila upendeleo.

Taarifa imeongeza kusema kuwa wote wanaokimbia migogoro wana haki sawa ya kupitishwa kwa usalama chini ya mkataba wa umoja wa mataifa na bila ya kujali rangi ya hati zao za kusafiria au ngozi zao.

XS
SM
MD
LG