Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 04, 2022 Local time: 10:44

Uvamizi wa Russia huenda ukasababisha raia wa Ukraine milioni 4 kukimbia nchi yao


Wakimbizi wa Ukraine wakiwasili kituo cha teni cha Zahonyi karibu na mpaka wa Hungary-Ukraine, Feb. 27, 2022.(Photo by Attila KISBENEDEK / AFP)

Uvamizi na Russia nchini Ukraine huenda ukawalazimisha raia wa Ukraine takriban milioni 4 kukimbia nchi yao, Umoja wa Mataifa umeeleza wiki hii, ukipelekea kuwepo mgogoro mbaya sana wa wakimbizi kuliko yote barani Ulaya kuwahi kutokea zaidi ya miaka 70 iliyopita.

Kulingana na taarifa ya Jumapili ya shirika la Umojawa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, raia wa Ukraine 368,000 wamevuka mpaka na kuingia katika nchi jirani na idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka.

Poland – pamoja na Moldova, Romania, Slovakia na Hungary – zimelegeza masharti ya COVID-19 mpakani kuruhusu raia wa Ukraine wanaokimbia uvamizi wa Russia.

Serikali ya Poland ilitangaza kufungua mipaka yake na imesema haitahitaji watu kuwa na nyaraka rasmi.

“Tutamsaidia kila mtu. Hatutaacha kumsaidia mtu yeyote,” Idara ya kusimamia mpaka Poland imesema.

Kulingana na shirika la habari la AP, msururu wa magari huko Medyka, mpaka wa Poland na Ukraine yalikuwa urefu wa kilomita 15.

Maia Sandu, Rais wa Moldova, alitweet Alhamisi, “ Serikali imefungua vituo vya muda karibu na eneo la Palanca na Ocnita. Mipaka yetu iko wazi kwa raia wa Ukraine ambao wanataka njia salama kuvuka kwenda nchi nyingine au kukaa hapa hapa.”

Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban, mmoja wa washirika wa Rais wa Russia Vladimir Putin, amesema katika mkutano na waandishi wa habari wiki hii, Hungary itaruhusu wakimbizi waingie hata kama hawana nyaraka.

Maelfu ya wakimbizi tayari wameshavuka Hungary kwenye mpaka wenye urefu wa maili 85 na Ukraine. Hungary pia imesema Jumamosi haitazuia vikwazo vyovyote dhidi ya Russia.

Wakimbizi hao ni wanawake, watoto na wazee kwa sababu Rais wa Ukraine Volovymyr Zelenskyy amepiga marufuku mapema wiki hii wanaume walio na umri wa kuweza kutumikia jeshi kuondoka nchini.

Nchini Marekani, Utawala wa Biden uumeliomba Bunge kutoa dola bilioni 6.4 kuipa Ukraine, baadhi ya fedha hizo zitatumika kwa misaada ya kibinadamu.

Sehemu ya habari hii chanzo chake ni mashirika ya habari ya AP na Reuters

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG