Odinga amefananisha uchaguzi na vita, akisema kuwa wapiganaji kabla ya kuingia kwenye medani ya vita ni nuksi kufanya mapenzi, kitendo ambacho kinaweza kupelekea kushindwa vita hivyo.
“Tunakwenda vitani na ni lazima tusipoteze nguvu zetu zote kabla ya siku ya mapambano, ambayo ni Agosti 8,” amesema huko Homa Jumatatu.
“Asipatikane yoyote kati yetu ambaye atafanya mapenzi katika kilele cha uchaguzi.”
Raila aliwataka hasa wanaume kujizuia kufanya mapenzi, akisema itapelekea baadhi yao kushindwa kwenda kupiga kura siku ya Agosti 8.
Amewaambia wanawake wasikubali kufanya mapenzi na waume zao usiku wa Agosti 7.
“Wanawake wote wakatalieni waume zenu haki zao za ndoa katika kilele cha siku ya kupiga kura,” amesema mwanasiasa huyo.