Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Februari 09, 2023 Local time: 02:15

Raila asema lazima mabadiliko ya katiba Kenya yafanyike


Rais Uhuru Kenyatta (kushoto) na Makamu wa Rais William

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga, amesema kwamba mabadiliko ya katiba ya nchi hiyo hayawezi kuepukika kwa namna yoyote ile na kwamba hata walio madarakani hawawezi kuzuia kura ya maoni kuhusu katiba, ili kusuluhisha matatizo yanayo ikabili nchi hiyo.

Odinga anasema kwamba hakuna katiba iliyo kamilika kote duniani lakini ipo haja ya kuibadili katiba ya Kenya ili kupunguza mzigo wa maisha kwa raia, kwani imedhihirika kwamba katiba ina makosa.

Akihutubia wafuasi wake katika kaunti ya Migori, magharibi mwa Kenya, Odinga amesema kwamba muda wa kubadilisha katiba ya Kenya umewadia, akilinganisha maoni ya wanao pinga mabadiliko ya katiba ya nchi hiyo na vilio vya chura, visivyo mzuia ng’ombe kunywa waji.

Odinga amesema kwamba kamati iliyoteuliwa kukusanya maoni jinsi ya kuwwaunganisha wakenya wote baada ya mkutano kati yake na Uhuru Kenyatta, imeanza kazi na kwamba ripoti yake itatumika kumaliza matatizo ya Wakenya daima.

“Tuna katiba mpya ndio. Lakini ilivyo na katiba zingine kote dunaini, zinahitaji kufanyiwa majaribio baada ya miaka nane ili kujua kilicho sawa na kile ambacho si sawa kwa watu wetu. Tunastahili kujua iwapo ugatuzi unawwanufaisha raia, iwapo baraza la mawaziri ni kubwa, maswala ya mazingira na mengineyo. Hii ndio sababu tunataka mabadiliko ya katiba na hakuna anayeweza kuzuia wazo ambalo mda wake umefika. Mda wa kubadilisha katiba yetu ni sasa na kama hutaki, jiondoe. Tutakutana uwanjani” amesema Odinga

Mjadala wa mabadiliko ya katiba

Hoja ya kutaka katiba ya Kenya kubadilishwa imepata umaarufu baada ya nyongeza ya ushuru wa mafuta ya asilimia 16, iliyobadilishwa na rais Uhuru Kenyatta hadi asilimia 8, miongoni mwa hatua nyingine za ushuru, ili kukithi mahitaji ya kifedha ya Kenya.

Wakenya wanapendekeza mabadiliko ya katiba ili kupunguza idhadi ya magavana, maseneta, wabunge, waakilishi wa bunge la kaunti miongoni mwa maafisa wengine wa kisiasa, kwa msingi kwamba mzigo wa kuwalipa mshahara ni mzito.

Wachambuzi wa siasa za Kenya wanasemaje?

Lakini Michael Agwanda, mchambuzi wa siasa za Kenya, anataka wanasiasa kusema ukweli kwamba nia ya kubadilisha katiba ni kubadilisha mfumo wa uongozi, unaomnyang’anya rais madaraka na kuyaweka kwa bunge, mfumo ambao utahakikisha kwamba wanasiasa wote wanaoshiriki uchaguzi mkuu, wanapata nafasi serikalini hata wanaposhindwa.

“Jinsi katiba yetu ilivyo sasa, yule anayepata kuwa president anachukua madaraka yote. Ni heri tuwe na katiba inayowatambua hata wale ambao wamepoteza katika uchaguzi ili kuzuia vurugu kila baada ya uchaguzi” amesema Agwanda

Msimamo wa Kenyatta na Ruto

Wanasiasa wanaomuunga Raila Odinga, wanaunga mkono mabadiliko ya katiba, huku wale wanaomuunga mkono naibu wa Rais William Ruto, wakipinga.

Hata hivyo, wanaomuunga mkono naibu wa rais William Ruto, wanasema kwamba mabadiliko ya katiba yanastahili kufanyika tu kwa kuzingatia namna ya kupunguza mzigo wa maisha kwa mwananchi na wala sio kuhusu madaraka.

Rais Uhuru Kenyatta kwa upande wake, amekaa kimya kuhusu mabadiliko ya katiba.

Imetayarishwa na Kennes Bwire, Sauti ya Amerika, Washington DC

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG