Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 04, 2023 Local time: 13:50

Shambulio la kigaidi Spain lauwa raia wa Ulaya, Mmarekani


Watu wakiwa katika huzuni baada ya shambulizi la kigaidi katika eneo la tukio hilo huko Barcelona

Raia mmoja wa Mmarekani amethibitishwa kuuawa kufuatia shambulio la kigaidi huko Barcelona.

Katika tukio hilo watu 14 waliuawa, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Rex Tillerson amesema Ijumaa.

“Nakiri kuwa sasa tumepokea taarifa hiyo na tumethibitisha kifo cha Mmarekani mmoja katika tukio hilo la kigaidi Spain, akiwemo katika wale waliouwawa,” amesema Tillerson. Hata hivyo Tillerson hakutaja jina la Mmarekani aliyeuawa katika shambulizi hilo.

Tillerson amesema serikali ya Marekani bado inafuatilia kupata uhakika juu ya majeruhi na vifo vingine” na ametoa rambirambi kwa wale waliouawa.

Serikali kadhaa za Ulaya zimethibitisha kuwa wananchi wa nchi hizo wameuawa au kujeruhiwa katika shambulizi hilo, ikiwemo Ufaransa na Itali.

Waziri wa Mambo ya Nje Jean-Yves Le Drian amesema Ijumaa kuwa Wafaransa 26 ni kati ya wale waliojeruhiwa. Amesema 11 kati yao wako hali mbaya.

Waziri Mkuu wa Itali Paolo Gentiloni amesema Wataliano wawili waliuawa katika shambulizi hilo ambalo gari lilitumika kuwagonga watu.

XS
SM
MD
LG