Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Februari 23, 2024 Local time: 19:34

Tillerson ataka GCC kumaliza mgogoro wa Qatar


Rex Tillerson
Rex Tillerson

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Rex Tillerson amesema itakuwa vigumu kwa Qatar kuteleza masharti yote waliotoa Saudi Arabia na washirika wake watatu.

Lakini Tillerson aliwasihi pande zote mbili kutafuta suluhu ya kudumu kumaliza mgogoro wa kidiplomasia katika nchi hizo za ghuba ya uajemi (GCC).

Katika taarifa yake siku moja baada ya Qatar kukataa madai kama hayana msingi na yanaathiri uhuru wake, Tillerson alisema kuna maeneo muhimu ambayo yanatoa msingi wa kuweza kuendeleza mashauriano ili kufikia suluhisho.

Tillerson hakusema ni masuala ya aina gani anayodhani yangepelekea Misri, Bahrain na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) pamoja na Saudi Arabia kufikia makubaliano na Doha.

Serikali hizo nne za nchi za kiarabu ambazo zilikata uhusiano wa kidiplomasia na Qatar zaidi ya wiki mbili zilizopita kwa madai kwamba Qatar imekuwa ikichochea ugaidi katika eneo na Kuwait kuwasilisha madai yao kwa Qatar wiki iliyopita ambaye ni msuluhishi wa pande hizo mbili.

Kati ya madai mengine kutoka kwa nchi hizo nne ni kwamba Qatar ifunge mtandao wa televisheni ya Al-Jazeera, ambayo ni chanzo cha muda mrefu cha mgogoro kati ya Qatar na majirani zake.

XS
SM
MD
LG