Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 02, 2023 Local time: 15:10

Putin atangaza Russia kusitisha ushirikiano wake kwenye mkataba wa nyuklia wa START


Rais Vladmir Putin ahutubia bunge mjini Moscow

Rais wa Russia Vladimir Putin ametangaza Jumanne kwamba Moscow ilikuwa inasitisha kushiriki kwenye Mkataba mpya wa START – mkataba pekee uliobaki wa kudhibiti silaha za nyuklia na Marekani – hii ikiongeza mivutano iliyopo na Washington juu ya vita nchini Ukraine.

Akiongea katika hotuba ya hali ya kitaifa, Putin pia alisema kwamba Russia ni vyema ijiweke tayari kuanza majaribio ya silaha za nyuklia kama Marekani inafanya hivyo, hatua ambayo huenda ikamaliza marufuku ya ulimwengu juu ya majaribio ya silaha za nyuklia ambayo imewekwa tangu enzi ya Vita Baridi.

Akielezea uamauzi wake kusitisha majukumu ya Russia chini ya New START, Putin ameishutumu Marekani na washirika wake NATO kwa uwazi kutangaza lengo la kuishinda Russia nchini Ukraine. Rais Putin amesema “Wanataka kuweka mkakati wa sisi kushindwa na kujaribu kupata viwanda vyetu vya nyuklia. Kwa hili, nimelazimika kutangaza hivi leo kwamba Russia inasitisha ushiriki wake katika mkataba wa START.

Narejea kusema, hatuondoki katika mkataba huu, hapana, tunasitisha ushiriki wetu.” Putin alihalalisha hatua yake nchini Ukraine kwa kuishutumu nchi za Magharibi kwa kuitishia Russia.

“Maafisa wa vikosi vya kitaifa wamekuwa wakipatiwa mafunzo katika vyuo vya Magharibi na shule, wao nchi za Magharibi wamekuwa wakiwapatia silaha. Nataka kusisitiza kwamba Kyiv ilifanya mazungumzo na Magharibi kuhusu usambazaji wa mifumo wa ulinzi wa anga, kupambana na ndege na vifaa vingine vizito kabla ya kuanza kwa operesheni maalum ya kijeshi.

Tunakumbuka majaribio ya utawala wa Kyiv kupata silaha za nyuklia, walizungumza kuhusu hili hadharani. Marekani na NATO haraka wamefungua vituo vya kijeshi karibu na mipaka ya nchi yetu,” amesema Rais Putin.

Putin aliwashukuru wakazi wa maeneo ya Ukraini wanayoyakalia kimabavu na kuapa kuendelea kufanya kazi ya kuyarejesha. “Maneno maalum kwa wakati wa Jamhuri za Donetsk na Luhansk, mikoa ya Zaporizhzhia na Kherson. Nyinyi wenyewe, marafiki zetu, kwa ajili yenu wenyewe na mustakbali wenu, mmefanya mamuzi thabiti, licha ya vitisho na ugaidi wa nazi mamboleo, katika hali ambapo hatua ya kijeshi inafanyika karibu sana na mlipo.

Lakini kulikuwa na hakuna kituo chochote kilicho na nguvu sana kuliko azma yetu kwa Russia na majumbani mwenu.” Wakati katika inatoa mamlaka kwa rais kutoa hotuba kila mwaka, Putin hajawahi kuhutubia hata mara moja mwaka 2022, wakati wanajeshi wake walipoingia nchini Ukraine na kupata athari kubwa. Hivi sasa hotuba yake imekuja siku chache kabla ya maadhimisho yam waka mmoja ya operesheni za kijeshi hapo Ijumaa.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG