Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 23, 2024 Local time: 08:32
VOA Direct Packages

Russia imetekeleza ukatili wa kibinadamu, asema Kamala Harris


Makamu rais wa Marekani Kamala Harris, na Chansela wa Ujerumani, Olaf Scholz,kwenye mkutano wa usalama mjini Munich, Ujerumani Feb 17,2023
Makamu rais wa Marekani Kamala Harris, na Chansela wa Ujerumani, Olaf Scholz,kwenye mkutano wa usalama mjini Munich, Ujerumani Feb 17,2023

Makamu wa rais wa Marekani Kamala Harris amesema Jumamosi kwamba utawala wa Biden umefikia uamuzi rasmi kwamba Russia imetekeleza ukatili dhidi ya  ubinadamu kwa uvamizi wake nchini Ukraine wa takriban mwaka mmoja.

Harris ambaye aliwahi kuwa mwendesha mashitaka alisema katika mkutano wa usalama mjini Munich kwamba wamekusanya ushahidi wa kutosha pamoja na kufahamu viwango vya kisheria, na kwa hivyo hawana shaka kwamba ukatili dhidi ya ubinadamu umetekelezwa.

Ameongeza kusema kwamba wale wote walioshiriki kwenye ukatili huo , pamoja na viongozi waliowaamuru watawajibishwa kwa mujibu wa sheria. Matamshi ya Harris yamekuja wakati viongozi wa mataifa ya magharibi wanakutana mjini humo ili kutathimini kuhusu vita hivyo vibaya zaidi barani Ulaya tangu kumalizika kwa vita vya pili vya dunia.

Washington inatumai kwamba itaweza kumtenga zaidi Rais wa Russia Vladimir Putin, pamoja na kuchukua hatua za kisheria, ili kuwawajibisha maafisa wa serikali, yake kupitia vikwazo pamoja na mahakama za kimataifa. Wakati huo huo rais wa Ukraine Volodymr Zelenskiyy wakati akihutubia mkutano huo wa Munich kwa njia ya video amesema kwamba hakuna njia nyingine ila ushindi wa taifa lake kwenye mapigano hayo. Amesema kwamba kila mara Russia inalenga silaha dhidi ya Ukraine, ni sawa na kuielekeza kwa jirani zake.

XS
SM
MD
LG