Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 07:21

Mihimili ya Serikali kuguswa na punguzo la mishahara Kenya


Rais Uhuru Kenyatta
Rais Uhuru Kenyatta

Tume ya kuratibu mishahara ya wafanyakazi wa Umma (SRC) Kenya imetangaza Jumatatu mfumo mpya wa mishahara ya maafisa wa ngazi za juu katika serikali akiwemo Rais na Naibu wake.

Wengine watakao guswa na mabadiliko hayo ni maspika wa mabunge mawili, wabunge, magavana, maseneta, wakilishi wa mabunge ya kaunti na maafisa wengineo. Mfumo huu unaanza kutekelezwa rasmi Septemba mwaka huu baada ya uchaguzi mkuu.

Mwenyekiti wa Tume hiyo Sarah Serem anaeleza kuwa huu mfumo mpya wa mishahara unapania kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma na hivyo basi hatua yake itaokoa takriban shilingi bilioni 8 kila mwaka kwa taifa na kupunguza kiwango cha mishahara kwa umma kwa asilimia 35.

Tume hiyo pia imeondoa mfuko wa marupurupu kwa viongozi wote yakiwemo marupurupu ya vikao vya bunge ambapo kila mbunge alikuwa akilipwa sh.5,000 kwa kila kikao.

Pia yalikuwepo marupurupu ya usafiri, marupurupu ya majukumu maalum anayotwikwa afisa fulani. Sasa patakuwa na mpangilio wa marupurupu utakaoainishwa kwa mshahara wao.

Punguzo la Mishahara

Rais: Sh1.4 milioni kutoka Sh1.65 milioni (punguzo la 18%)

Naibu Rais: 1.2 milioni kutoka 1. 4 milioni(punguzo la 14%)

Mawaziri: Sh924,000 kutoka Sh1.1 milioni(punguzo la 13%)

Makatibu Wakuu: Sh765,000 kutoka Sh874,000(punguzo la 12%)

Magavana: Sh924,000 kutoka Sh1.1 milioni(punguzo la 13%)

Wabunge: Sh621,000 kutoka Sh710,000(punguzo la 13%)

Maspika wa mabunge mawili: Sh1.16 milioni kutoka Sh1.30 milioni(punguzo la 11%)

Manaibu Spika: Sh924,000 kutoka Sh1.0 milioni(punguzo la 8.2%)

Viongozi wa Serikali na Upinzani Bungeni: Sh765,000 kutoka 1.020 milioni(punguzo la 25%)

Wawakilishi wa Wadi katika bunge la Kaunti: Sh144,000 kutoka Sh165,000(punguzo la 13%)

Mawaziri wa Serikali za Kaunti: Sh259, 875 kutoka Sh350,000(punguzo la asilimia 26%)

Mfumo huu unaanza kutekelezwa rasmi Septemba mwaka huu baada ya uchaguzi mkuu.

Mnamo Septemba 2015, akiwasilisha mswada bungeni, Ababu Namwamba, Mbunge wa Budalang’i alikuwa amependekeza kuwa kuwepo punguzo la asilimia 50 ya mishahara ya wabunge na maafisa wengine wa serikali.

Wale ambao wangeguswa na punguzo hilo lililopendekezwa ni pamoja na Rais na makamu wake, wabunge, spika wa mabunge yote mawili, majaji, makamishna, mawaziri na makatibu wakuu, magavana na maafisa wa kaunti.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:17 0:00

XS
SM
MD
LG