Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 04, 2024 Local time: 01:27

Prince William amuoa Catherine Middleton


Prince William akimbusu mkewe Kate, Duchess of Cambridge, Buckingham Palace, baada ya kuoana April 29, 2011, mjini London.
Prince William akimbusu mkewe Kate, Duchess of Cambridge, Buckingham Palace, baada ya kuoana April 29, 2011, mjini London.

Wanandoa wafurahisha umma uliohudhuria kwa busu mbili za kufuatana huku ndege za kivita za Uingereza zikipita juu

Mara baada ya ndoa:

**Prince William na mkewe Catherine, Duchess wa Cambridge, washikana mikono na kumfuata Malkia Elizabeth na familia zao ndani ya jumba la kifalme la Buckingham.

**Busu la kwanza halikutosha. Wananchi waliohudhuria wakaomba busu jingine, basi Prince William akainama na kumbusu tena mkewe huku ndege za jeshi la hewani la Uingereza zikipita juu.


Habari Kamili:

Wanandoa wapya Prince William na mkewe Catherine ambayo sasa watachukua vyeo vya Duke na Duchess wa Cambridge katika ufalme wa Uingereza, walijitokeza kutoka Westminster Abbey na kupokelewa na shangwe kubwa kutoka kwa maelfu ya watu waliokusanyika kushuhudia ndoa hiyo ya kihistoria.

Walipanda katika gari la wazi linalovutwa na farasi kuelekea Buckingham Palace kwa chakula cha mchana na Malkia Elizabeth. Hali ya hewa ilikuwa nzuri, jua maridadi likiwaka na anga zilizo wazi kabisa.

William na Catherine walikula viapo vya mke na mume katika sherehe iliyopendeza ambayo haijapata kuonekana Uingereza tangu mwaka 1981 pale walipoana wazazi wa Prince William yaani Prince Charles na hayati Princess Diana.

XS
SM
MD
LG