Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Juni 24, 2024 Local time: 03:51

Harusi ya Kifalme huwenda ikafufua uchumi wa Uingereza


Mwana mfalme William na mchumba wake Kate Middleton
Mwana mfalme William na mchumba wake Kate Middleton

Mji mkuu wa UIngereza, London umefurika na watu kutoka pembe mbali mbali za dunia kuhudhuria harusi ya mwana mfalme Willaim na Kate Middleton.

Maeneo yote mashuhuri ya kutembelea katika jiji hilo yamejaa. Wapiga picha wa televisheni kutoka nchi zote za dunia wanashindana kupata nafasi nzuri kuweza kufuatilia sherehe zote. Na kivutio kikuu kwa wote ni kanisa la Wesmister Abbey ambako mwana mfalme William na Kate Middleton wataingia kufunga ndoa.

Watali wengine laki 6 wanatarajiwa kufika London kujaribu angalao kuwaona bawna na bibi marusi.

Mambo haya yote yanachangia kuimarisha uchumi wa uingereza anasema Mark di Toro wa idara ya utali ya serikali, Tembelea Ungereza.

"Utawala wa kifalme kila mwaka unatuletea pauni milioni 500 katika uchumi. Hiyo ni tawi ya sekta yetu ya utamaduni na urathi wetu ambayo ni chanzo moja wapo ya kuu ya kuiuza uingereza, inayotuletea pauni milioni 4.6. lakini kwa siku yenyewe watali hao milioni moja ifdadi ya watakaotembelea London kwa siku hiyo ni lazima itatuletea karibu pauni milioni 50 kutokana na matumizi ya watali".

Serikali inadai kwamba harusi ya kifalme itachochea mwanzo wa faida bilioni 3.3 kwa uingereza ukichukulia sherhe za miaka 50 ya malkia baadae mwaka huu na michezo ya Olympic 2012. Hiyyo ni hatua muhimu ya kufufua uchumi.

XS
SM
MD
LG