Rais Obama aitembelea Kenya (1)
Rais Obama aitembelea Kenya (1)

5
Rais Barack Obama anaangalia maonyesho ya nishati ya jua alipotembelea Power Africa Innovation Fair, Jumamosi, Julai 25, 2015, mjini Nairobi. Ziara ya Obama nchini Kenya imelenga kwenye masuala ya biashara na uchumi, pamoja na usalama na ushirikiano wa kukabiliana na ugaidi.

6
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta anaongea wakati wa mkutano wa pamoja na Rais Barack Obama kwenye ikulu, Jumamosi, Julai 25, 2015, huko Nairobi, Kenya. Obama amelitaja bara la Afrika kuwa linasonga mbele.

7
Rais Barack Obama, kushoto, na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta wakiwapungia watu wakati wakiondoka kwenye mkutano wa kimataifa wa ujasiriamali kwenye jengo la Umoja wa mataifa, Jumamosi, Julai 25, 2015, mjini Nairobi. Ziara ya Obama Kenya imelenga kwenye masuala ya biashara na uchumi, pamoja na usalama na ushirikiano katika kukabiliana na ugaidi.

8
Rais Barack Obama anaangalia jinsi ya kufanya malipo kwa njia ya simu ya mkononi na matumizi ya nishati ya nguvu za jua wakati wa maonyesho ya Power Africa Innovation Fair, Jumamosi, Julai 25, 2015 mjini Nairobi. ziara ya Obama Kenya imelenga masuala ya biashara na uchumi, pamoja na usalama na ushirikiano katika kukabiliana na ugaidi.