Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 03, 2024 Local time: 18:16

Prague yakumbwa na huzuni ya shambulizi la bunduki chuo kikuu


Watu wakusanyika kuwakumbuka waathirika wa shambulizi la bunduki Prague, Czech.
Watu wakusanyika kuwakumbuka waathirika wa shambulizi la bunduki Prague, Czech.

Jamhuri ya Czech imetangaza siku ya maombolezo kote katika nchi hiyo ya Ulaya ya kati Desemba 23 kuwakumbuka waathirika wa shambulizi lililotekelezwa na mwanafunzi wa Czech mwenye umri wa miaka 24.

Watu wakusanyika kuwakumbuka waathirika wa shambulizi la bunduki Prague.
Watu wakusanyika kuwakumbuka waathirika wa shambulizi la bunduki Prague.

Mwanafunzi huyo alimpiga risasi baba yake, kisha kuua watu 14 na kuwajeruhi wengine 25 katika chuo kikuu cha Prague siku ya Alhamisi.

Eneo hilo lilizingirwa siku ya Ijumaa kwa uchunguzi.

Polisi walipata mkusanyiko mkubwa wa silaha katika jengo la Chuo Kikuu cha Prague Charles ambako mashambulizi yalifanyika.

Polisi hao walidokezwa mapema siku hiyo kuwa mshukiwa alikuwa akielekea Prague kutoka mjini kwake katika mkoa wa Kladno nje ya mji mkuu kwa nia ya kujitoa uhai.

Idara ya Usalama ililifunga eneo hilo karibu na jengo la chuo, katika wilaya ya kihistoria yenye shughuli nyingi mkabala na mto Prague Castle kwenye barabara maarufu inayoelekea Old Town Square.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters.

Forum

XS
SM
MD
LG