Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 13, 2024 Local time: 12:50

Polisi 2 wauawa katika lindo la kanisa Kenya


Wanajeshi wakilinda maeneo ya pwani kutokana na kuzuia vitendo vya kigaidi
Wanajeshi wakilinda maeneo ya pwani kutokana na kuzuia vitendo vya kigaidi

Maafisa wawili wa polisi wauawa baada ya kupigwa risasi na washukiwa wa ujambazi.

Tukio hilo limetokea Jumapili katika kanisa moja huko Ukunda kusini mwa pwani ya Kenya saa nne asubuhi.

Mwandishi wa idhaa ya Kiswahili VOA ameripoti kuwa Kamishina wa Polisi wa kaunti ya Kwale, kutswa Olaka amesema kuwa maafisa hao walikuwa katika kanisa la eneo hilo wakilinda usalama wa raia.

Maafisa hao walipigwa risasi na watu waliokuwa wamebebwa na bodaboda kisha wakatoroka na bunduki za maafisa hao.

Wote wawili wamefriki njiani wakikimbizwa hospitalini.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu Kenya

XS
SM
MD
LG