Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 04:25

Marekani, Uingereza zalaani kauli za uchochezi Kenya


Polisi wakiwatawanya waandamanaji Nairobi, Octoba 2, 2017.
Polisi wakiwatawanya waandamanaji Nairobi, Octoba 2, 2017.

Polisi Kenya wamewatawanya waandamanaji kwa kutumia mabomu ya kutoa machozi Nairobi, Mombasa na Kisumu.

Muungano wa upinzani wa Nasa ulikuwa umeitisha maadamano hayo kuishinikiza Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kufanya mabadiliko katika safu ya maafisa wake kabla ya marudio ya uchaguzi wa urais Octoba 26, 2017.Maafisa hao wanashutumiwa na Nasa kuhusika na kuvuruga uchaguzi uliopita.

Wagombea wa nafasi hiyo ya urais Uhuru Kenyatta na Raila Odinga pia wanashindana juu ya pendekezo la kufanya mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi ili kuzuia Mahakama ya Juu kuwa na uwezo wa kubatilisha matokeo ya uchaguzi mara nyengine.

Chama cha Kenyatta cha Jubilee kimepeleka bungeni pendekezo hilo wiki iliyopita lakini Umoja wa Upinzani wa Nasa chini ya Odinga wamesema hawatashiriki mpaka mabadiliko hayo yasitishwe

Baada ya mkutano wao na IEBC, wanadiplomasia wa Uingereza na Marekani wamelaani “kauli za kisiasa zenye uchochezi” zinazotolewa na wanasiasa na kusema kuwa inavuruga uwezo wa tume kufanya kazi yake ya kuendesha uchaguzi mpya.

Shughuli za kibiashara zilisitishwa na ghasia hizo wakati upinzani wenye wafuasi wengi katika eneo hilo la Kisumu kupambana na polisi wakati wa maandamano hayo.

Kenya ni mshirika mkubwa wa Kenya ambayo imekuwa ikiyumbishwa na uvunjifu wa amani mara kwa mara.

Pia ni nchi tajiri kwa kuwa na kipato cha juu cha wananchi wake katika Afrika Mashariki na milango mkuu wa biashara na usafirishaji.

XS
SM
MD
LG